Jopo la watu saba lililoteuliwa na muungano wa Azimio kuwakilisha kwenye mazungumzo ya kuleta uwiano kati yao na mrengo wa Kenya Kwanza  umemtaja wakili Paul Mwangi  kama katibu wa Pamoja , Prof Makau Mutua na  Jeremiah Kioni  kama wasaidizi  kabla ya  kuanza kwa mazunguzo hayo.

Mwenyekiti wa jopo hilo Otiende Amollo ametanagza kuwa tayari wamebuni  rasimu ya mpango utakaosaidia  kuyaelekeza mazungumzo hayo pindi yatakapoanza.

Aidha amepinga uteuzi wa mbunge wa Eldas Aden Keynan kwenye timu ya kenya kwanza akidai kuwa ni mbunge wa azimio la umoja.

Amollo aliandamana na katibu wa chama cha ODM Edwin Sifuna ,maseneta Enoch Wambua (Kitui) na Ledama Ole Kina (Narok), sawa  na wabunge  David P’Kosing (Pokot South), Millie Odhiambo (Suba North) and Amina Mnyanzi (Malindi).

Amesisitiza kuwa maswala nyeti wanayotaka yashughulikiwe na mazungumzo hayo ni Pamoja na kupunguzwa kwa bei ya unga ,mafuta,umeme ,uchunguzi wa sava za tume ya uchaguzi nchini IEBC ,mchakato wa kubuni tume ya iebc uweze kuwashirikisha pande zote mbili ,heshima kwa demokrasia na nidhamu kwa vyama vya kisiasa.

April 13, 2023