BY ISAYA BURUGU,18TH APRIL,2023-Muungano wa Azimio la Umoja hivi leo umeonya kwamba hautashiriki kabisa hoja iliyoandaliwa na Wabunge wa Kenya Kwanza katika azma ya kuunda Kamati ya Vyama Viwili.
Wakizungumza katika Kituo cha Stephen Kalonzo Musyoka (SKM) jijini Nairobi, muungano unaoongozwa na Raila Odinga ulimshutumu Rais William Ruto kwa kutenda kwa nia mbaya kwa kutoshauriana nao kuhusu mswada unaokuja wa pande mbili.
Taarifa hiyo iliyodai kuwa Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah hakushauriana na upinzani wakati wa kuandaa mswada huo, ilisomwa na Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka.
“Hoja hiyo inafichwa kama zao la vyama viwili wakati uongozi wa Azimio la Umoja Bungeni haukuwa na taarifa wala kushauriana juu yake,” Kalozo alisoma.
Mrengo wa Kenya Kwanza ulikuwa umewasilisha hoja katika Bunge la Kitaifa, kutaka kubuni kamati ya pande mbili.