BY ISAYA BURUGU,28TH FEB,2023-Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini imetabiri kuwa mvua itashuhudiwa katika baadhi ya maeneo haswa yale ya Bonde la ufa.
Baadhi ya maeneo ambako kunatabiriwa kuwa na mvua mapema mwezi ujao ni ziwa Victoria ,kusini na kati mwa bonde la ufa.Mashariki ya juu na magharibi mwa rift valley.
Idara hiyo inadokeza kuwa maeneo yanayoshudia mvua kwa sasa yataendelea hivyo kuanzia hivi leo hadi Machi tarehe sita.
Maeneo mengine nchini yataendelea kushuhudia jua kali,nyuzi joto maeneo mengi zikitarajiwa kuwa chini ya digrii kumi.