Baadhi ya wabunge wamefanya kikao na wanahabari hii leo kulalamikia kucheleweshwa kwa mgao wa hazina ya ustawi wa maeneobunge CDF.

Wakiongozwa na mbunge wa Rarieda Otiende Amollo,wabunge hao wamedai kuwa hakuna eneobunge lolote ambalo limepokea fedha huku wakiikashifu serikali kwa kutomiza ahadi yake ya kutoa fedha hizo kwa maeneobunge tarehe 20 mwezi desemba mwaka jana.

January 9, 2024