Wakaazi wa mji wa Narok wamejiunga na viongozi wa Azimio la umoja kufanya mandamano ili kuishinikiza serikali ya Kenya Kwanza kupunguza gharama ya maisha.
Wakizungumza na waandishi wa habari, wakaazi hao wameshutumu serikali ya kwa kuongeza bei ya bidhaa muhimu kama vile mafuta ilhali waliahidi kuwa watapunguza gharama ya maisha wakati wa kampeni zao.
Mamia ya vijana walijitokeza katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi, ili kushiriki katika maandamano yaliyotangazwa siku ya leo na Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga.
Idadi ya maafisa wa polisi nayo iliongezwa maradufu ili kudumisha hali ya usalama na utulivu kwenye jiji hilo.
Odinga aliwaongoza wananchi katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kamukunji ambapo ameapa kukusanya sahihi zaidi ya milioni 10 ili kuanza kile anachodai kuwa ni mapinduzi dhidi ya serikali ya Rais William Ruto.
Polisi Kule Kisii wameambiwa na wanainchi, Murife don’t run. Njooni tusalamiane na tujuane. #SabaSabaMarchForOurLives #Maandamano pic.twitter.com/KTFz3qpRkZ
— Azimio TV (@AzimioTv) July 7, 2023
Breaking News: Wednesday 12th July 2023 we have another Rally at Kamkunji and Nationwide Demonstrations.
Vrooom! #SabaSabaMarchForOurLives #Maandamano
— Azimio TV (@AzimioTv) July 7, 2023