Huku ulimwegu ukiadhimisha siku ya afya duniani, baadhi ya wakaazi wa Narok wameeleza kuwa huduma ya afya ya jamii SHA haifanyi kazi,na hivyo basi inakua ngumu kupata matibabu kwa wakati ufaao.

Wakaazi hao wakizungumza na waandishi wa Habari wa kituo hiki cha Radio Osotua, wameiomba serikali ya Narok itoe rasilmali za matibabu na ununuzi wa dawa,wakisema kuwa mara nyingi wanalazimika kuenda kwenye hospitali za kibinafsi kupimwa na kupata dawa ambazo wanauziwa kwa bei ghali.

Vile vile wakaazi hao wameitaka serikali hiyo ya Narok kuanzisha mpango wa madaktari kuwafikia wagonjwa nyumbani,wakisema kuwa wengi wao wanakosa uwezo wa kufika kwenye vituo vya afya kutokana na hali ngumu ya maisha.

April 7, 2025

Leave a Comment