Njuguna Bajeti

Waziri wa hazina kuu ya kitaifa Njuguna Ndung’u siku ya Alhamisi aliwasilisha makadirio ya bajeti ya taifa katika kipindi cha kifedha cha mwaka 2023/24 kwenye vikao vya bunge la taifa. Bajeti hii ambayo ndiyo ya kwanza chini ya utawala wa serikali ya Kenya Kwanza imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kuu kutokana na masuala mengi yaliyokuwa yamependekezwa.

Waziri Ndung’u wakati akiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo ya shilingi trilioni 3.7 amesema kuwa serikali inapania kukusanya ushuru wa shilingi trilioni 2.96 ikijumuisha misaada na ruzuku ambayo ni sawa na asilimia 18.2 ya Pato la Taifa. Aidha fedha zinazotarajiwa kukusanywa kama ushuru pekee ni shilingi Trilioni 2.57 sawa na asilimia 15.8 ya pato la taifa.

Ndung’u ameongeza kuwa kubuniwa kwa bajeti hiyo kulifuata sheria kwani wakenya walishiriki na kutoa maoni yao kuhusu masuala ambayo yalihitaji kushughulikiwa katika bajeti huku akidai kuwa mapendekezo yaliyotolewa na wananchi yameangaziwa vilivyo katika bajeti hiyo. Uchumi wa taifa aidha unatarajiwa kuimarika na kupanuka kwa asilimia 5.5 mwaka 2023, kutoka asilimia 4.8 ya mwaka 2022 na kudumisha kasi hiyo katika miezi sita iliyosalia.

Wafanyabiashara wadogo wafaidi.

Wafanyabiashara wadogo wadogo, wanawake na pamoja na vijana humu nchini, pia wanatarajiwa kunufaika na fedha zaidi ili kuwawezesha kujiimarisha hasa wale walio katika sekta ya uzalishaji.

Katika makadirio ya bajeti, wizara ya hazina ya kitaifa imetenga mgao wa shilingi Bilioni 10 kwa mpango wa Hazina ya Hustler (Hustler Fund) Shilingi Milioni 300 kwa biashara ndogo na za kadri hasa katika sekta ya utengenezaji, na shilingi Milioni 182.8 na milioni 175 kwa hazina ya biashara ya wanawake pamoja hazina ya biashara na maendeleo ya vijana mtawalia.

Next Show
John Waicua

Anga za Osotua Asubuhi

Show Time

Wednesday
7:00 am-7:15 am
June 15, 2023