Narok County

Baraza la mawaziri katika kaunti ya Narok limeidhinisha bajeti ya miradi ya maendeleo katika kaunti hii, kuelekea katika mwaka ujao wa kifedha, kabla ya mapendekezo hayo kuwasilishwa katika bunge la kaunti ili kuidhinishwa.

Katika kikao cha leo kilichoongozwa na gavana Patrick Ntutu, mawaziri waliwasilisha ripoti zao za miradi ya maendeleo na jinsi wanapanga kuafikia maendeleo katika wizara zao.

Gavana Ntutu kwenye taarifa iliyochapishwa baada ya kikao hicho, amesisitiza kujitolea kwa serikali yake katika kufanikisha miradi ya maendeleo kwa wananchi wa kaunti hii.

https://twitter.com/NarokCountyGvt/status/1650849372005867520?s=20

April 25, 2023