Bei ya unga huu nchini inatarajiwa kuenda chini juma lijalo. Haya ni kwa mujibu wa Rais William Ruto ambaye ameeleza kwamba serikali inafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kwamba bei ya bidhaa muhimu inapungua kote nchini.

Akizungumza katika eneo la Mavoko baada ya kuzindua mradi wa usambazaji wa maji katika kaunti ya Machakos, Rais Ruto pia aliwaomba viongozi wa upinzani kuwa watulivu na kuirhusu serikali kutekeleza majukumu ya kushusha gharama ya Maisha, akiwasuta kuwa walichangia pakubwa kwa mfumko wa bei ya unga katika kipindi kilichopita cha uongozi.

https://twitter.com/WilliamsRuto/status/1646861933830717440?s=20

Wakati hayo yakijiri,mahakama Kuu nchini imesitisha kwa muda uamuzi wa serikali ya Kenya kuwapa kandarasi wakulima wa taifa la  Zambia kulima mahindi kwa ajili ya kuuzwa nchini Kenya.

Jaji wa Mahakama hiyo Mugure Thande alitoa agizo la kumzuia Waziri wa Kilimo Mithika Linturi kutekeleza Mkataba wa Maelewano kati ya Kenya na Zambia, utakaowaruhusu wakulima nchini Zambia kuzalisha mahindi na kuyasafirisha humu nchini.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya Chama cha Wakulima nchini kuwasilisha kesi dhidi ya serikali kuhusu uamuzi wa kupeana kandarasi hiyo, wakitaja hatua hiyo kama isiyo na mantiki na inayokiuka katiba ya taifa la Kenya.

April 14, 2023