Bunge la kitaifa limeidhinisha mchakato wa kutumwa kwa maafisa 1000 wa polisi nchini Haiti, chini ya ujumbe wa kulinda amani ulioidhinisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN).
Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Idara ya Utawala na Usalama wa Ndani na Kamati ya Kudumu ya Seneti kuhusu Usalama wa Kitaifa, Ulinzi na Uhusiano wa Kigeni kwa pamoja waliidhinisha ujumbe utakaopelekea polisi wa Kenya kutumwa katika taifa hilo mwaka ujao ili kukabiliana na magenge ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakivamia mji mkuu wa Haiti,Port-au-Prince.
Akiwa mbele ya kamati ya pamoja ya usalama mnamo Novemba 9, 2023, Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome alisema kuwa maafisa hao watatumwa kwa awamu na zoezi la mchujo limefanywa ili kubaini maafisa watakaoshiriki misheni hiyo.