Jeshi la Kongo limewashutumu waasi wa M23 kwa kuwaua takriban raia 50 katika mji wa mashariki wa Kishishe. Haya yanajiri huku kukiwa na taarifa za mauaji ya watu wengi kufuatia kuanza tena kwa mapigano, huku usitishaji mapigano uliokubaliwa wiki iliyopita ukionekana kuporomoka.…
Rais wa Rwanda Paul Kagame amemtuhumu mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi kwa kutumia migogoro ya mashariki mwa DRC kama kisingizio cha kuchelewesha uchaguzi. Akizungumza bungeni jana jioni, Kagame alisema dunia nzima inailaumu Rwanda kwa migogoro hiyo, wakati Tshisekedi…
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekwenda Marekani, katika ziara ya kwanza ya kiserikali tangu Rais Joe Biden alipoingia madarakani. Uhusiano baina ya marais hao ulianza kwa kusuasua, hadi kufikia hatua ya Ufaransa kumrudisha nyumbani balozi wake mjini Washington baada ya Marekani kuipiku…
Mazungumzo yanayolenga kuleta amani mashariki mwa DRC yamefanyika jijini Nairobi ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria mazungumzo hayo ili kutafuta suluhu ya kudumu. Viongozi kutoka jumuiya ya kikanda, Jumuiya ya Afrika Mashariki wanajaribu kuharakisha juhudi zinazoendelea za kikanda ili kufikia amani na usalama endelevu…
Tume ya taifa ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika Desemba 20, 2023, licha ya kuzorota kwa usalama mashariki mwa nchi hiyo. Tangazo la tume hiyo, CENI lililotolewa hii leo limekuja wakati waasi wakiendeleza harakati…
Rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA Gianni Infantino, amejibu ukosoaji unaotolewa kwa Qatar kuhusu madai ya ukiukwaji haki za binaadam akisema huu ni unafiki wa mataifa ya Magharibi. Infantino ameyasema hayo siku moja kabla ya ufunguzi wa mashindano ya Kombe la…
Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta amewaomba wapiganaji katika maeneo tofauti ya taifa la Congo DR, kukumbatia njia mbadala za kutatua tofauti zao, na kusitisha mapigano yanayoendelea katika taifa hilo. Uhuru alikua akizungumza baada ya kuhudhuria kikao cha mashauriano na kutafuta njia za kurejesha…
Rais wa Marekani Joe Biden hii leo amewasili kwenye mji wa mwambao wa Sharm el-Sheikh nchini Misri kuhudhuria mkutano wa kilele wa Mabadiliko ya Tabianchi wa COP27 unaotafuta makubaliano ya kudhibiti taathira za kuongezeka kwa kiwango cha joto duniani. Wajumbe wa mkutano…