Umoja wa Mataifa umeonya kuwa mlipuko wa kipindupindu nchini Haiti unaenea kwa kasi, huku idadi ya maambukizi ikiongezeka maradufu na kufikia wananchi wapatao 2,000 katika muda wa siku chache zilizopita. Wizara ya afya nchini Haiti imeripoti angalau vifo 41 kati ya Oktoba…
Mataifa ya Umoja wa Ulaya yanapania kukubaliana kuhusu msimamo wao wa pamoja, katika mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo suala linaloleta mvutano la fidia ya fedha kwa uharibifu unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika mataifa masikini…
Umoja wa Mataifa umesema kwamba msaada wa kimataifa wa chakula kwa taifa la Somalia ndiyo sababu pekee iliyopunguza hatari ya njaa katika taifa hilo linalozongwa na machafuko. Hata hivyo shirika la Mpango wa Chakula Ulimwenguni la umoja huo WFP, limetahadharisha kwamba ikiwa…
Shirika la afya duniani WHO limesema janga la covid-19 pamoja na vita na migogoro ni masuala yaliyorudisha nyuma juhudi za kuimarisha afya na ustawi wa wanawake pamoja na watoto. Kwa mujibu wa data za WHO zilizowasilishwa katika mkutano wake wa kilele mjini…
Serikali ya Marekani imetangaza hatua ya kupeleka silaha zaidi Ukraine zilizo na thamani ya Yuro milioni 725. Kulingana na taarifa kutoka katika Ikulu ya White House silaha hizo ni pamoja na mifumo ya makombora ya masafa marefu ya HIMARS, magari ya kivita…
Watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wamewaua watu 12 kwa kuwakatakata kwa mapanga katika kijiji kimoja Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo kwa miaka mingi limekuwa likikumbwa na machafuko kutoka kwa makundi yaliyojihami kwa silaha. Akizungumza na shirika la habari la…
Nchi 26 za Afrika zilipiga kura kuunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa la kupinga kura za maoni zenye utata wa Moscow katika mikoa minne ya Ukraine ambayo ilitangaza kuwa ni sehemu ya Urusi. Nchi 19 hazikupiga kura hiyo, ikiwa ni pamoja…
Wakaazi wa eneo la Amhara nchini Ethiopia ambalo lilichukuliwa tena na wanajeshi wa serikali hivi karibuni wamewashutumu wapiganaji kutoka eneo la Tigray kwa unyanyasaji ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela. Wilaya ya Raya Kobo ilishikiliwa kwa wiki tano na vikosi vya…