Vikao vya UNEA 6

Wajumbe 5,000 Kuhudhuria Kongamano la Sita la UNEA Lililoanza Jijini Nairobi.

Awamu ya sita ya kongamano la Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA), imeng’oa nanga asubuhi ya leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) eneo la gigiri katika kaunti ya Nairobi. Kongamano hilo la siku…

Aliyekuwa bingwa wa mbio za Marathon Kelvin Kiptum azikwa.

Aliyekuwa bingwa wa mbio za Marathon Kelvin Kiptum amezikwa hii leo katika eneo la Naiberi kaunti ya Uasin Gishu. Hafla ya mazishi ya mwanariadha huyo ilihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini akiwamo rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua…

Kenya yapiga hatua kubwa katika ulipaji wa madeni yake.

Rais William Ruto amesema kuwa Kenya imepiga hatua kubwa katika kujiondoa kwenye orodha ya mataifa yasiyotilia mkazo ulipaji wa madeni yake. Akiwahutubia waandishi wa habari katika eneo la Naivasha baada ya kukamilika kwa mkutano wa mawaziri, kiongozi wa taifa amesema kwamba taifa…

Jaji mkuu Martha Koome ashikilia kwamba uhuru wa mahakama hautaingiliwa kwa namna yoyote

Jaji mkuu Martha Koome ameshikilia kwamba uhuru wa idara ya mahakama hautaingiliwa kwa namna yoyote. Kwenye kikao na waandishi wa habari baada ya kufanya mkutano na rais William Ruto huko Naivasha, Koome hata hivyo amesema kuwa idara hiyo iko tayari kufanya mazungumzo…

joto kali kuendelea nchini

Joto Kali kuendelea kuathiri Maeneo Mengi ya Taifa – Idara ya Utabiri Yasema

Vipindi vya joto kali vinatarajiwa kuendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya taifa juma hili, kulingana na taarifa kutoka Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga nchini. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa joto litazidi kupanda na kufikia viwango vya juu zaidi ya nyuzijoto 30…

UDA

UDA Yaunga Mkono Azma ya Raila Odinga Kugombea Uenyekiti wa AU.

Chama Tawala cha UDA kimetangaza rasmi kuiunga mkono azma ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Muungano wa Umoja wa Afrika (AU). Katibu wa Kitaifa wa UDA, Cleophas Malala, alitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, akifafanua…

Biashara ya Pombe haramu Mlima Kenya

Polisi Walaumiwa Kwa Kutositisha Biashara ya Pombe Haramu Mt. Kenya.

Maafisa wa usalama katika ukanda wa Mt. Kenya wameshutumiwa kwa utepetevu katika jitihada za kukabiliana na biashara ya pombe haramu. Kauli hii imetolewa na viongozi mbalimbali wa ukanda wa mlima Kenya, wakiongozwa na Naibu wa Rais Rigathi Gachagua. Wakizungumza katika Shule ya…

Rais Ruto na Mkewe

Rais Ruto na Mkewe Kuzuru Marekani Mwezi Mei Kwa Mwaliko wa Rais Biden.

Rais William Ruto na mkewe, Bi Rachel Ruto, wanatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Marekani mwezi Mei mwaka huu, kufuatia mwaliko maalum kutoka kwa Rais Joe Biden na mkewe, Bi Jill Biden. Ziara hii imewekwa wazi katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Mawasiliano…