Serikali ya kaunti ya Narok yatoa jumla ya shilingi 579,280 kwa Wanafunzi walemavu.

Serikali ya kaunti ya Narok imetoa jumla ya shilingi 579,280 kwa Wanafunzi 16 ambao ni walemavu ili kufanikisha ndoto yao ya elimu kupitia ofisi ya watu wanaoishi na ulemavu kaunti ya Narok. Akizungumza mjini Narok mkurugenzi wa watu wanaoishi na ulemavu kaunti…

Mtu mmoja afariki basi mbili za shule zikigongana kaunti ya Kirinyaga

BY ISAYA BURUGU,5TH APRIL,2023-Mtu mmoja ameripotiwa kufariki huku wanafunzi kadhaa wakijeruhiwa baada ya basi mbili za shule kugongana ana kwa ana kwenye barabara ya Kagio kuelekea Baricho kaunti ya Kirinyaga leo asubuhi.Wakaazi waliokuwa karibu walikimbia kwenye eneo la tukio kujaribu kuwaokoa manusura…

Rais William Ruto aanza ziara ya siku tatu nchini Rwanda.

Rais William Ruto aliwasili katika taifa la Rwanda kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili. Rais Ruto na mwenyeji Rais Paul Kagame wanatarajiwa kujadiliana kuhusu maswala ya ushirikiano kati ya mataifa haya mawili, ikiwa ni pamoja na miradi ya usalama wa chakula,…

Raila asema hakukutana na Rais Ruto kabla ya kusitisha maandamano.

Kinara wa upinzani Raila Odinga amefutilia mbali taarifa kuwa kulikua na mkutano kati yake na Rais William Ruto kabla ya tangazo la kusitisha maandamano siku ya Jumapili. Odinga ambaye alihutubia waandishi wa habari kabla ya mkutano wa wajumbe wa muungano wa Azimio…

Mwili wa mtoto aliyetoweka wiki jana huko Nyamira wapatikana kwenye Kisima

BY ISAYA BURUGU,4TH APRIL,2023-Polisi katika Kaunti Ndogo ya Manga, kaunti ya Nyamira wanachunguza kisa ambapo mwili wa mtoto wa miaka 11 wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ekoro, kaunti ndogo ya Nyamira Kusini ulipatikana ndani ya kisima kilicho kwenye…

Rais Wiliam Ruto atangaza kuwa wakongwe kupata mgao wa fedha zao kabla ya watumishi wa umma kuanzia Juni Mosi

BY ISAYA BURUGU  4TH APRIL,2023-Rais Wiliam Ruto ruto ametangaza kuwa kuanzia tarehe moja mwezi Juni mwaka huu mgao wa fedha zilizotengwa wazee na makundi mengine hitajika katika jamii zitaanza kutolewa kabla ya mishahara ya watumishi wa umma.Akizungumza katika kongamano la kulinda maslahi…

Musalia Mudavadi awarai vijana kukumbatia Teknolojia kupunguza ukosefu wa ajira.

Mkuu wa mawaziri nchini Musalia Mudavadi, amewataka wahusika wote katika sekta ya Teknolojia na mawasiliano pamoja na vijana wenye ujuzi wa masuala ya teknolojia kunyakua fursa zinazopatikana katika anga ya kidijitali ili kupunguza idadi ya watu wasio na ajira, na pia kuliweka…

Shule ya upili ya Mukumu yafungwa baada ya vifo vya wanafunzi wawili kutokana na chakula.

Shughuli za masomo katika shule ya upili ya Mukumu Kaunti ya Kakamega zimesitishwa baada ya shule hiyo kufungwa kwa muda usiojulikana kufuatia maradhi yaliyowaandamana wanafunzi shuleni humo na kusababisha kuaga dunia kwa wanafunzi wawili. Inakisiwa kwamba wanafunzi hao walikula chakula kilichokua kimeathirika,…