Mpango wa usimamizi wa mbuga ya Maasai Mara wazinduliwa rasmi.

Gavana wa Narok Patrick Ntutu, Waziri wa mazingira Soipan Tuya Pamoja na Waziri wa Utalii Penina Malonza, wameongoza shughuli za uzinduzi wa mpango wa usimamizi wa mbuga ya maasai mara kutwa ya leo. Viongozi hao wamekariri kujitolea kwa idara zao kuendelea kutunza…

Malumbano kati ya serikali na upinzani yaendelea, kila mwamba ngoma akivuta kwake.

kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga, ameeleza kwamba maandamano yaliyoratibiwa kuandaliwa siku ya Jumatatu juma lijalo yataendelea kama yalivyoratibiwa. Katika kikao na waandishi wa habari alasiri ya Leo, Odinga amesema kwamba muungano huo umepata kufahamu kuhusu njama ya viongozi…

NCCK lamtaka rais William Ruto kufanya mazungumzo na Raila Odinga ili kusitisha maandamano.

Baraza la madhehebu mbalimbali nchini NCCK limemtaka rais William Ruto kufanya mazungumzo na kinara wa upinzani Raila Odinga ili kusitisha maandamano. Wakiwahutubia waandishi wa habari huko Limuru, viongozi hao wameeleza kuwa kuna haja ya kutumia njia mbadala ya kutafuta suluhu ya matatizo…

Waumini wa dini ya Kislamu waanza kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan

BY ISAYA BURUGU 23RD MARCH,2023-Waumini wa dini ya Kislamu kote nchini hivi leo wameungana na wenzao duniani kuanza kipindi cha mwezi wa mfungo mtukufu wa Ramadhani.Katika kipindi hiki,waislam hufunga, kusali, na kutoa msaada kwa wasiojiweza katika jamii. Mkuu wa maimamu kaunti ya…

Rais Ruto ashuhudia kuapishwa kwa makatibu wakuu wandamizi 50

BY ISAYA BURUGU,23RD MARCH,2023- Rais William Ruto hivi leo ameshuhudia kuapishwa kwa Makatibu Wakuu 50 wa Tawala katika hafla iliyofanyika Ikulu.Wateule hao wa CAS walitangazwa kwenye gazeti la serikali Jumatano na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei. Mawasiliano ya awali kutoka…

Rais Ruto kuzuru kaunti za Kisii na Nyamira kuanzia Alhamisi.

Rais William Ruto anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya kikazi kwa siku tatu katika kaunti za Kisii na Nyamira Pamoja na Maeneo bunge ya Kuria magharibi na Kuria Mashariki kuanzia hapo kesho. Kulingana na msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, ratiba ya Rais itaangazia…

Rais William Ruto akashifu maandamano ya Raila Odinga dhidi ya serikali.

Rais William Ruto amekashifu maandamano ya Raila Odinga dhidi ya serikali yaliyopangwa kufanyika Jumatatu na Alhamisi kila wiki. Katika maoni mafupi ya kuchekesha Mkuu wa Nchi ameonyesha matumaini kwamba siku hizo mbili hivi karibuni zitakuwa siku ambazo zitarekodi idadi kubwa zaidi ya…

KCCB lataka mazungumzo yafanyike kati ya Rais William Ruto na Raila Odinga.

Baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki limetaka mazungumzo yafanyike kati ya Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ili kuepusha mzozo unaojitokeza. Wakihutubia wanahabari Maaskofu hao wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo askofu mkuu Martin Kivuva, wamemsihi Rais Ruto atimize…