IPOA yachunguza visa viwili vya madai ya ukatili wa polisi vilivyotokea Kisumu na Nairobi.

Mamlaka Huru ya kutathmini utendakazi wa Polisi IPOA inachunguza visa viwili vya madai ya ukatili wa polisi vilivyotokea Kisumu na Nairobi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali. Kulingana na taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa Mamlaka hiyo, Anne Makori, maafisa wa IPOA waliotumwa…

Wito watolewa kwa wakaazi wa Narok kupanda miti kwa wingi,Kenya ikiungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya upazni wa miti

BY ISAYA BURUGU,21ST MARCH,2023-Kenya imeungana na ulimwengu hivi leo kuadhimisha siku ya upandaji miiti duniani wito ukitolewa kwa wakaazi wa Narok kupanda miti kwa wingi ili kupiga jeki juhudi za serikali kuafikia miti bilioni 15. Naibu gavana wa kaunti ya Narok Tamalinye…

Kenya Kwanza wakashfu mandamano ya Azimio ya Jumatatu ukiyataja kuwa ujangili

 BY ISAYA BURUGU,21ST MARCH,2023-Viongozi wa Kenya Kwanza wamekashfu  mandamano ya hiyo jana yaliyoandaliwa na mungano wa Azimio la umoja .Katika kikao na wandishi habari viongozi hao wakiongozwa na gavana wa Embu Cicil MBarire wanasema kuwa mandamano hayo yaliyipelekea Kenya kupoteza mamilioni ya…

Gavana Nyong’o alaani uharibifu uliotekelezwa wakati wa Maandamano Kisumu.

Gavana wa kaunti ya Kisumu Prof. Anyang’ Nyong’o amelaani vitendo vya uharibifu wa mali vilivyoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya kaUnti hiyo, kufuatia maandamano yaliyoandaliwa ili kulalamikia ongezeko la gharama ya Maisha. Kupitia taarifa aliyochapisha jioni ya leo, Gavana Nyong’o ameeleza kusikitishwa…

Rais Ruto: Hakuna mkenya aliye juu ya sheria

Rais William Ruto amekariri kuwa atajikita kwenye katiba na sheria za taifa katika utendakazi wake, akieleza kwamba kutekeleza jambo lolote nje ya katiba kutalielekeza taifa katika njia isiyofaa. Akizungumza baada ya kuongoza hafla ya kuapishwa kwa wakili mkuu Shadrack Mose katika ikulu…

Mbunge Opiyo Wandayi na seneta Stewart Madzayo wakamatwa Nairobi

BY ISAYA BURUGU,20TH MARCH,2023-Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi  na seneta  wa Kilifi  Stewart Madzayo  wamekamatwa jijini Nairobi katika mandamano ya Azimio yanayoendelea. Mandamano hayo yameandaliwa kupinga kupanda kwa gharama ya Maisha.Taarifa zasema kuwa wawili hao  walikamatwa katika jumba la mikutano la KICC …

Usalama waimarishwa Nairobi na kwingineko nchini Azimio wakifanya mandamano

BY ISAYA BURUGU,20TH MARCH,2023-Usalama umeimarishwa katika sehemu mbali mbali nje na ndani ya jijini kuu Nairobi siku ambayo mungano wa Azimio la umoja umepanga kufanya mandamano.Uchunguzi uliyofanywa na Redio Osotua umebaini kuwa katika sehemu ambazo kwa kawaida ulinzi hua ni mkali katika…

Linturi awaomba wakulima Narok kuuza mahindi yao ili kuepuka hasara.

Waziri wa kilimo nchini Mithika Linturi, amewarai wakulima walio na mahindi katika maghala yao kuuza mahindi hayo, ili kuepuka hasara ya kupungua kwa bei, mara serikali itakapoanza uagizaji wa mahindi kutoka katika mataifa ya nje. Akiwahutubia wenyeji wa eneo la Talek Narok…