Walichosema Viongozi siku ya kuwasherehekea wanawake.

Taifa la Kenya limeungana na ulimwengu mzima hii leo, katika kuiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, inayotoa nafasi ya kuyasherehekea mafanikio ya wanawake pasi na kuwabagua kwa misingi ya kikabila, kitamaduni, kiuchumi au kisiasa. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu, ilikuwa…

Kamati ya Bunge yaidhinisha uteuzi wa Susan Jemutai kama Naibu Gavana wa CBK.

Kamati ya fedha na Mipango katika bunge la kitaifa, imeidhinisha uteuzi wa Dkt Susan Jemutai Koech kama naibu gavana wa pili wa Benki Kuu nchini (CBK) Dkt. Jemutai ambaye aliwahi kuhudumu kama katibu mkuu katika wizara ya jumuia ya Afrika Mashariki, alikuwa…

Viongozi wa Azimio la Umoja waitaka serikali kutimiza ahadi walizotoa wakati wa kampeni.

Baadhi ya viongozi wa Azimio la Umoja sasa wanaitaka serikali kutimiza ahadi zao walizotoa wakati wa kampeni badala ya kuilaumu serikali iliyopita. Wabunge hao wakiongozwa na Edwin Sifuna walisema utawala unaoongozwa na rais William Ruto umekuwa ukinyooshea kidole utawala uliopita badala ya…

Wito watolewa kwa kina mama kuwa watu wenye sala na upendo katika jamii siku zote.

wito umetolewa kwa kina mama kuwa watu wenye sala na upendo katika jamii siku zote. Akizungumza alipoungana na wanawake kusherehekea siku ya wanawake duniani, msimamizi wa miradi katika jimbo la Eldoret Abigael Mahindu amewataka kina mama kuwa chombo cha sala katika familia…

Polisi waanzisha uchunguzi huku mwanamme mmoja akifariki kwa njia tatanishi kwenye nyumba ya msanii DJ Fantxo

BY ISAYA BURUGU,8TH MARCH 2023– Maafisa wa polisi  wanachunguza  kifo cha kutatanisha cha  mrembeshaji nyumba  Geoffrey Mwathi, aliyefariki baada ya kuanguka  kutoka kwa orofa ya kumi ya jumba la  Redwood kwa njia isiyojulikana. Mwathi,mwenye umri wa  23, anasemekana  kufariki baada ya kuanguka …

Akina mama Narok watoa wito kwa serikali ya kaunti kuwasaidia kifedha kuinua biashara

BY ISAYA BURUGU,8TH MARCH,2023-Huku Kenya ikiungana na ulimwengu kuadhimisha siku ya Akina mama  duniani leo,akina mama katika kaunti hii ya Narok wameitaka serikali kuwasaidia katika kuwapiga jeki kiuchumi kwa kuinua biashara zao ndogo ndogo. Kwa mjibu wa Sila Letiet ambaye ni mama,…

Naibu chansela wa chuo cha Meru Prof. Romanus Odhiambo arejeshwa kazini.

Siku moja baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Meru kuandaa maandamano wakilalamikia hatua ya kupewa likizo ya lazima kwa naibu chansella wa chuo hicho Prof. Romanus Odhiambo, Waziri wa elimu nchini Ezekiel Machogu ameagiza kurejeshwa kazini mara moja kwa naibu huyo…

Makamishena 20 wahamishwa, 15 wasalia huku manaibu kamishena 12 wakipandishwa ngazi.

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amefanya mabadiliko chungu nzima katika wizara yake, baada ya kuwahamisha makamishena 20 hadi maeneo mbadala, na kuwapandisha cheo manaibu kamishena 12 hadi katika ngazi ya kuwa makamishena, huku makamishena 15 wakisalia katika vituo vyao vya…