Mahakama ya Rufaa Kutoa Uamuzi Kuhusu Ada ya Nyumba Tarehe 26 Januari.

Mahakama ya Rufaa nchini imeongeza muda wa kutoa uamuzi kuhusu kesi inayohusu ada ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu, hivyo kuwalazimu Wakenya wanaotozwa ada hizo kusubiri kwa muda zaidi kujua hatma ya malipo yao. Uamuzi huo umesogezwa hadi tarehe 26 mwezi…

Hatutababaika Wala Kutishika, Maafisa wa Idara ya Mahakama Wamjibu Rais.

Jaji mkuu nchini Martha Koome amevunja kimya chake kufuatia kauli ya viongozi wa serikali dhidi ya mahakama. Katika notisi iliyochapishwa kwa wafanyakazi wa idara ya mahakama, jaji Koome amewataka wafanyakazi wote wa mahakama kutoyumbishwa na yeyote katika kazi yao, na kuwataka kuendelea…

MAHAKAMA YASITISHA MAENDELEO

Rais Ruto na Naibu Wake Waikosoa Mahakama kwa Kusimamisha Maendeleo.

Ufa mkubwa umeanza kujitokeza waziwazi kati ya idara ya mahakama na viongozi wakuu serikalini, huku viongozi hao wa kisiasa wakitoa kauli kali dhidi ya maamuzi yanayotolewa na mahakama. Miongoni mwa viongozi wa hivi karibuni kutoa kauli za kukosoa mahakama ni Naibu wa…

Mwaka mpya

Shangwe na Nderemo Zatawala Watu Wakiukaribisha Mwaka Mpya 2024.

Shangwe na nderemo zilitawala maeneo mbalimbali ya ulimwengu usiku wa kuamkia leo, huku watu wakisherehekea kwa furaha kuingia kwenye mwaka mpya wa 2024. Sherehe hizi za kukaribisha mwaka mpya ziliandaliwa katika pembe tofauti za ulimwengu, huku watu wakichagua njia mbalimbali za kusherehekea…

Gavana Natembeya apendekeza wakaazi wa Trans Nzoia kutumia mahindi kulipia bima ya NHIF

30TH DEC,2023-Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya amependekeza mpango mpya ambapo wakazi watachangia gunia moja la kilo 90 za mahindi kila mwaka ili kujiandikisha katika Hazina ya Kitaifa ya Bima ya Afya (NHIF). Akihutubia wakazi katika kambi ya matibabu ya bure huko…

Utafiti wa shirika la TIFA waonyesha kuwa wakenya wengi hawajaridhishwa na utenda kazi wa serikali.

 29TH DEC,2023- Wakenya hawajaridhishwa na utendakazi wa jumla wa Rais William Ruto na utawala wake mwaka mmoja madarakani.Haya ni kulingana na kura ya maoni ya mwisho wa mwaka iliyofanywa na kampuni ya utafiti ya Infotrak ambayo matokeo yake yalitolewa Ijumaa. Wakenya walioshiriki…

Matokeo ya mtihani wa KCSE mwaka huu kutangazwa wiki ya pili ya Januari- Waziri Machogu

28TH DEC,2023- Matokeo ya mtihani wa kidato cha nee KCSE mwaka huu  yatatangazwa wiki ya pili ya Januari, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesema. Machogu alisema wanafunzi 903,260 waliofanya mtihani wao wa mwisho wa elimu ya sekondari mnamo Novemba 2023 watajua hatima…

Kundi la vijana lafanya mandamano Nairobi kuunga mkono ushuru wa nyumba

28TH DEC,2023-Kundi la vijana hivi leo limemiminika katika mitaa ya  Kati ya Biashara ya Nairobi (CBD) wakipinga zuio la mahakama dhidi ya Mradi wa Nyumba za gharama nafuu unaoendelezwa na serikali. Waandamanaji hao waliandamana kupitia barabara ya Moi, Tom Mboya na Kenyatta…