Wabunge wa magharibi waahidi kushirikiana licha ya mirengo yao ya kisiasa.

Wabunge kutoka eneo la magharibi wamekutana na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi ambapo wameahidi kufanya kazi pamoja kwa maendeleo ya eneo hilo. Wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa muungano wa wabunge wa Kanda ya Magharibi John Waluke walikutana na Mudavadi katika kikao…

Serikali yapania kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na Korea kusini.

Rais William Ruto amesema serikali itapanua uhusiano wa kiuchumi na Korea Kusini ili kubuni nafasi za biashara na ajira kwa wakenya. Akizungumza wakati wa mkutano nchini Korea Kusini, Rais Ruto alisema Kenya itashirikiana na Serikali ya Korea Kusini kufungua fursa katika teknolojia,…

Rais William Ruto awasili katika taifa la Korea Kusini kwa ziara rasmi.

Rais William Ruto amewasili katika taifa la Korea kusini kwa ziara rasmi katika taifa hilo ambapo anatarajiw akuandaa mashauriano na rais Yoon Suk Yeol. Rais Ruto aliwasili katika taifa la Kora Kusini adhuhuri ya leo Jumanne 22.11.2022, na anatarajiwa kuendeleza mashauriano na…

Maandalizi ya mitihani ya kitaifa Narok yanoga shule zikiweka hatua za lala salama

BY ISAYA BURUGU 22ND NOV 2022-Huku mitihani ya kitaifa ikiratibiwa kuanza kote nchini katika muda wa wiki moja ijayo shule ziko kwenye harakati za mwisho mwisho kujiandaa kwa kipindi hicho cha mitihani. Shule ya upili ya wasichana ya Kilgoris haijaachwa nyuma katika…

Kaunti ya Kisumu yazindua mpango wa utoaji huduma msingi za kiafya kwa njia ya kuzuia

BY ISAYA BURUGU 22ND NOV 2022-Serikali ya kaunti ya Kisumu imezindua  mkakati wa utoaji huduma msingi za kiafya  unaotilia maanani  kuzuia magonjwa  huku washirika  wakiitisha kutengewa fedha Zaidi za mpango huo.Mpango huo wa miaka miwili  unatokana na na mpango wa kitaiafa wa…

Peter Ndegwa ateuliwa kuongoza kamati ya kukabiliana na ukame nchini.

Rais William Ruto ameunda Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na jinamizi la Ukame, kamati itakayoongozwa na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom Peter Ndegwa. Kulingana na Notisi ya Gazeti la Serikali iliyochapishwa hii leo, uundaji wa kamati hiyo ulitokana…

Rais William Ruto apeleka ujumbe wa Amani katika taifa la DRC Congo.

Rais William Ruto amesisitiza kwa mara nyingine kujitolea kwa taifa la Kenya katika kulipiga jeki taifa la DRC Congo na kulisaidia ili kukabiliana na changamoto nyingi zinazolikumba taifa hilo. Rais Ruto aliyasema haya katika hotuba yake nchini DRC alikowasili ili kufanya mashauriano…

Mmiliki wa jumba lililoporomoka katika eneo la Ruaka atiwa mbaroni.

Jengo lenye ghorofa tano liliporomoka katika eneo la Ruiru kaunti ya Kiambu saa chache baada ya kuhamishwa kwa wapangaji Zaidi ya mia moja kutoka kwa jengo hilo. Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi, pamoja na Zimamoto waliongoza shughuli za uokoaji Jumapili baada ya…