Rais Ruto azindua mradi wa ujenzi wa barabara ya kilomita 40 huko mtwapa.

Rais William Ruto hii leo amezindua mradi wa ujenzi wa barabara ya mtwapa-kilifi ambayo inatarajiwa kurahisisha usafiri baina ya kaunti za Mombasa na Kilifi. Rais Ruto amesema kuwa barabara hiyo ya kilomita 40 itapunguza kero la msongamano wa magari sawa na kuimarisha…

EPRA yapanga kampeni kuwasadia wakenya kujiepusha na mikasa ya gesi.

Mamlaka ya kudhibiti bei ya mafuta humu nchini EPRA imezindua msururu wa kampeni za kuwahamasisha wananchi kuhusu matumizi yanayofaa ya kawi ili kuepuka ajali za mara kwa mara. Mamlaka hiyo imeanzisha kampeni hiyo ili kuwaonya wananchi dhidi ya kufyonza mafuta katika lori…

Washukiwa sita wa uhalifu wazuiliwa katika kituo cha polisi cha kasarani.

Maafisa wa polisi katika eneo la Kasarani wamewatia nguvuni washukiwa sita wa ujambazi wanaohuishwa na visa vya uhalifu katika maeneo mbalimbali jijini Nairobi.Washukiwa hao sita wa ujambazi wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kasarani. Washukiwa hao walikamatwa  wakati wa msako wa usalama…

Rais Ruto azindua kiwanda cha kutengeneza chuma katika kaunti ya Kwale.

Rais William Ruto amezindua rasmi kiwanda cha kutengeneza chuma cha Devki katika eneo la kinango kaunti ya Kwale. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ruto amesema kuwa serikali itaunga mkono kiwanda hicho ambacho kimegharimu shilingi bilioni 30 ili kutoa nafasi Zaidi za ajira…

Mbunge wa Sirisia John Waluke aachiliwa huru kwa dhamana ya shilinngi milioni 10 pesa taslimu

BY ISAYA BURUGU,18TH NOV 2022-Mbunge wa eneo bunge la Sirisia  John Waluke  ameachiliwa kwa dhaman aya shilingi milioni kumi pesa taslim na mahakama ya rufaa  kusubiri kusikilizwa kwa rufaa aliyowasilisha dhidi ya hukumu yake ya miaka 67.Haya yanajiri  baada ya Waluke mwezi…

Serikali yatoa mwelekeo kuhusu namna wakenya watakavyoomba mikopo katika hazina ya ‘Hasla’

BY ISAYA BURUGU ,18TH NOV,2022-Waziri wa vyama vya ushirika Simon Chelugui ametoa mwelekeo kuhusu hazina ya hasla ambayo rais Wiliam Ruto anatarajiwa kuzindua mwishoni mwa mwezi huu. Akizungumza na wandishi Habari afisini mwake,Waziri amesema kuwa masharti ya utoaji mikopo hiyo ambayo kiwango…

MP. John Kiarie

Mazingira: Wabunge waidhinisha hoja ya upanzi wa miti barabarani.

Wabunge katika bunge la kitaifa wamekubaliana kwa kauli moja kuiidhinisha hoja ya mbunge wa Dagoretti John Kiarie, itakayowalazimu wanakandarasi kuipanda miti iliyong’olewa wakati wa ujenzi wa barabara. Hoja hii ambayo sasa inasubiri hatua za mwisho ili kuwa sheri, pia imeitaka serikali kuweka…

Ezekiel Machogu

Waziri wa elimu aahidi uadilifu wakati wa mitihani ya kitaifa.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amesisitiza utayari wa serikali katika kuifanikisha mitihani ya kitaifa inayotarajiwa kuanza baadae mwezi huu. Akizungumza katika Kaunti ya Kisumu alipokutana na Wakuu wa shule na wakurugenzi wa elimu katika kaunti hiyo, Waziri machogu alitoa hakikisho kuwa uadilifu…