Aden Duale

Duale, Murkomen na Wahome wajiuzulu kutoka kwa nyadhifa zao bungeni.

Waziri Mteule wa Ulinzi Aden Duale amemwandikia Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula waraka wa kujiuzulu kama Mbunge wa eneobunge la Garissa mjini, kama mojawapo ya njia kujiandaa kuchukua wadhifa wake mpya. Wengine waliotoa taarifa za kujiuzulu ni pamoja na seneta…

Gavana patrick Ntutu azindua shehena ya pili ya dawa.

Gavana wa Narok Patrick Ntutu amezindua shehena ya pili ya dawa ambayo itasambazwa kwa hospitali na zahanati mbalimbali katika kaunti ya Narok. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo katika hospitali ya rufaa ya Narok Ntutu  amedokeza kuwa serikali yake inapania kuimarisha huduma za…

Egerton University Strike

Mahakama ya Nakuru yasitisha mgomo wa wahadhiri wa Chuo kikuu cha Egerton.

Mahakama ya Ajira mjini Nakuru imeamuru kusitishwa mara moja kwa mgomo wa wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Egerton ili kutoa mwanya kwa mazungumzo kati ya pande husika. Katika uamuzi wake siku ya Jumanne 25.10.2022, Jaji Hellen Wasilwa ameagiza usimamizi wa chuo hicho…

Kazi mtaani imeisha

Rais William Ruto atupilia mbali mpango wa Kazi mtaani.

Rais William Ruto amevunja mpango wa kazi mtaani ambao ulikua ukitoa nafasi za kazi za kusafisha kwa vijana, na badala yake kusema kuwa vijana sasa watahusishwa katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu. Akizungumza katika mtaa wa Soweto mashariki eneobunge la kibera…

Inspekta jenerali wa polisi mteule Japheth Koome kuhojiwa tarehe 8 mwezi ujao.

Inspekta jenerali wa polisi mteule Japheth Koome anatarajiwa kufika mbele ya kamati za bunge la seneti na lile la kitaifa kwa zoezi la kupigwa msasa kabla ya kuidhinishwa kutwaa wadhfa huo. Koome atafika mbele ya kamati hizo tarehe 8 mwezi ujao. Kulingana…

Penina Malonza atemwa nje kama waziri mteule wa utalii.

Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Uteuzi imewasilisha ripoti ya zoezi la msasa wa mawaziri wateule 24 siku chache baada ya zoezi hilo kukamilika.Kamati hiyo imetupilia mbali uteuzi Penina Malonzo kama waziri mteule wa utalii huku mawaziri wateule waliosalia wakiidhinishwa na wabunge.…

LSK na rais Ruto

LSK yaunga mkono msimamo wa Rais Ruto kuhusu mauaji ya kiholela.

Chama cha Wanasheria nchini LSK Kimeeleza kuunga mkono msimamo wa Rais William Ruto dhidi ya mauaji kiholela na ukiukaji wa haki za binadamu, huku wakipendekeza kuundwa kwa tume ya uchunguzi itakayoshughulikia kesi za aina hii. Wanasheria hao walitoa mapendekezo haya katika kikao…

Gladys Chania na Maurice Mbugua waachiliwa kwa dhamana ya Ksh.1M kila mmoja.

Mwanasiasa wa Kiambu Gladys Chania na mshukiwa mwenza Maurice Mbugua wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja pesa taslimu kila mmoja. Chania na Mbugua wanashtakiwa kwa kupanga mauaji ya kikatili ya mumewe, mfanyabiashara George Mwangi. Idara ya Upelelezi wa Jinai ilikuwa imewasilisha…