Inspekta jenerali wa polisi mteule Japheth Koome kuhojiwa tarehe 8 mwezi ujao.

Inspekta jenerali wa polisi mteule Japheth Koome anatarajiwa kufika mbele ya kamati za bunge la seneti na lile la kitaifa kwa zoezi la kupigwa msasa kabla ya kuidhinishwa kutwaa wadhfa huo. Koome atafika mbele ya kamati hizo tarehe 8 mwezi ujao. Kulingana…

Penina Malonza atemwa nje kama waziri mteule wa utalii.

Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Uteuzi imewasilisha ripoti ya zoezi la msasa wa mawaziri wateule 24 siku chache baada ya zoezi hilo kukamilika.Kamati hiyo imetupilia mbali uteuzi Penina Malonzo kama waziri mteule wa utalii huku mawaziri wateule waliosalia wakiidhinishwa na wabunge.…

LSK na rais Ruto

LSK yaunga mkono msimamo wa Rais Ruto kuhusu mauaji ya kiholela.

Chama cha Wanasheria nchini LSK Kimeeleza kuunga mkono msimamo wa Rais William Ruto dhidi ya mauaji kiholela na ukiukaji wa haki za binadamu, huku wakipendekeza kuundwa kwa tume ya uchunguzi itakayoshughulikia kesi za aina hii. Wanasheria hao walitoa mapendekezo haya katika kikao…

Gladys Chania na Maurice Mbugua waachiliwa kwa dhamana ya Ksh.1M kila mmoja.

Mwanasiasa wa Kiambu Gladys Chania na mshukiwa mwenza Maurice Mbugua wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja pesa taslimu kila mmoja. Chania na Mbugua wanashtakiwa kwa kupanga mauaji ya kikatili ya mumewe, mfanyabiashara George Mwangi. Idara ya Upelelezi wa Jinai ilikuwa imewasilisha…

IPOA yaanzisha uchunguzi kufuatia mauaji ya mwanahabari wa pakistan.

Mamlaka huru ya utendakazi wa polisi IPOA imesema kuwa itawachukulia hatua za kisheria maafisa waliohusika na mauaji ya watu mbalimbali humu nchini. Kwenye kikao na waandishi wa habari, mwenyekiti wa mamlaka hiyo Ann Makori amedokeza kuwa IPOA inaunga mkono hatua ya rais…

Maasai Mara

Kamati maalum kutatua mizozo ya wanyamapori na binadamu eneo la Maasai Mara.

Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu ameahidi kubuni kamati maalum ya watu 30 itakayokuwa na jukumu la kusuluisha mizozo kati ya wanyama pori na binadamu katika mbuga ya kitaifa ya Maasai Mara. Ntutu ambaye alikua akizungumza katika eneo la sekenani siku…

Hustler Fund kuzinduliwa rasmi mwezi Disemba.

Rais William Ruto amefichua kuwa atazindua mradi wa mikopo na akiba wa Hustler Fund tarehe 1 Desemba 2022.Katika hotuba yake kwa taifa wakati wa maadhimisho ya sherehe za 59 za mashujaa, rais aliweka bayana kuwa maswali mengi yameulizwa kuhusu ahadi ya Hustler…

Gavana Ntutu aahidi kukarabati barabara zaidi katika maeneobunge ya Narok ili kurahisisha usafiri.

Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu amesema kuwa serikali yake inapania kukarabati barabara Zaidi katika maeneobunge ya Narok ili kurahisisha usafiri.Akizungumza wakti wa hafla ya maadhimisho ya mashujaa katika shule ya msingi ya DEB eneo la Kilgoris, Ntutu amesema kuwa…