Gavana wa Narok Patrick Ntutu awaonya magenge ya watu wanaowahangaisha wakaazi wa Narok

 BY ISAYA BURUGU,12TH DEC 2023-Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ntutu amehaidi kushirikiana na vikosi vya usalama kuwakamata wahalifu mjini Narok. Ntutu akizungumza katika madhimisho ya siku ya Jamhuri katika shule ya msingi ya Suswa Narok mashariki ameshutumu hatua ya wahalifu kuwavamia…

Rais William Ruto atangaza kuwa serikali itakomesha mahitaji ya viza kwa wageni wanaozuru nchini kutoka kote duniani kuanzia Januari 2024.

Rais William Ruto ametangaza kuwa serikali itakomesha mahitaji ya viza kwa wageni wanaozuru nchini kutoka kote duniani kuanzia Januari 2024. Rais aliyasema haya wakati wa sherehe za miaka 60 za Jamhuri katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi. Mkuu wa nchi alidokeza kuwa…

Waziri wa Kawi aonya kuhusu kukatika kwa umeme tena ikiwa uwekezaji unaofaa hautatekelezwa.

Waziri wa Kawi Davis Chirchir ameonya kuhusu kukatika kwa umeme tena nchini kote ikiwa uwekezaji unaofaa hautaelekezwa katika kuimarisha usambazaji wa umeme kote nchini. Kulingana na Chirchir, njia za usambazaji umeme nchini zimejaa kupita kiasi, jambo ambalo linaendelea kuzidisha kupotea kwa umeme…

UMEME

Huenda Kuna Watu Wanatatiza Mitambo ya Umeme JKIA – Waziri Murkomen.

Waziri wa Uchukuzi nchini Kipchumba Murkomen, sasa anasema kwamba huenda kuna mipango ya makusudi ya kuhitilafiana na mitambo ya nguvu za umeme katika uwanja wa ndege wa JKIA jijini Nairobi. Kulingana chapisho kwenye ukurasa wake wa X, Waziri huyo amesema kwamba hulka…

EACC yatoa wito wa ushirikiano kati ya tume hiyo na wananchi.

Tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC imetoa wito wa ushirikiano kati ya tume hiyo na wananchi ili kukabili visa vya ufisadi humu nchini. Akizungumza katika kaunti ya Murang’a wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya kupambana na ufisadi ulimwenguni, mwenyekiti wa…

Vijana

Vijana Nchini Wahimizwa Kukumbatia Kazi zilizo Kwenye Nyenzo za Kidijitali.

Kiongozi wa taifa Rais William Ruto, amewataka vijana kukumbatia nafasi za ajira zinazopatikana kwenye mifumo ya kidijitali, na kujipatia kipato cha kuimarisha maisha yao ya siku kwa siku. Akizungumza katika hafla ya Youth Connect Africa Katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi, kiongozi…

Rais Wiliam Ruto asisitiza msimamo wa utawala wake kuendelea kuwekeza katika vijana.

BY ISAYA BURUGU,8TH DEC 2023-Rais William Ruto hivi leo ameongoza  gwaride la kufaulu kwa zaidi ya wahitimu 10,000 katika chuo cha NYS huko Gilgil.Wahitimu hao wanajumuisha wanaume 6,861, 3,660 na watu wenye ulemavu 47 ambao ni sehemu ya timu iliyoajiriwa Mei mwaka…

Margaret Nyakang'o

Margaret Nyakang’o Apata Afueni Baada ya Mahakama Kusitisha Kushtakiwa Kwake.

Mdhibiti wa bajeti nchini, Margaret Nyakang’o, amepata afueni baada ya Mahakama Kuu nchini kutoa agizo la kusitisha kushtakiwa kwake hadi pale kesi iliyowasilishwa na Mbunge wa Mugirango Magharibi, Mogaka Musyoki, itakapoamuliwa mwezi Mei mwaka kesho. Musyoki aliwasilisha kesi mahakamani kupinga kukamatwa na…