Wanachama wa Kamati ya shughuli za Bunge waidhinishwa tayari kuanza kazi.

Bunge la Kitaifa alasiri ya leo limeidhinisha majina ya wanachama wake wa Kamati ya shughuli za Bunge, tayari kwa kuanza rasmi kwa shughuli za bunge hilo siku ya kesho. Spika Moses Wetangula amewaagiza wanakamati hao kuanza shughuli zao mara moja, kuanda hoja…

SERIKALI YA KAUNTI YA NAROK KUANZA KUWASAIDA WALIOATHIRIWA NA NJAA.

Wakenya wapatao 240,000 katika kaunti ya Narok wanakumbwa na makali ya njaa baada ya kushuhudiwa kwa vipindi virefu vya jua na ukame unaokumba kaunti 23 kote nchini. Ni kutokana na hali hii ambapo viongozi wa serikali ya kaunti ya Narok wakiongozwa na…

Kenya yaungana na ulimwengu kusherehekea siku ya mtoto wa kike duniani.

Wenyeji wa kaunti ya Narok  wametakiwa kuhakikisha kuwa swala la ukeketaji linatokomezwa kikamilifu.Wito huu umetolewa huku Kenya ikiungana na ulimwengu hii leo kuadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani. Kwa mujibu wa Mihele Kishoyian ambaye ni mwanaharakati wa kupigania haki za mtoto…

Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka apinga uingizaji wa vyakula vya GMO humu nchini.

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amepinga vikali hatua ya kuondolewa kwa marufuku ya utengenezaji na uingizaji wa vyakula vya kisaki au GMO. Akiwahutubia waaandishi wa habari,Kalonzo amesema kuwa sayansi imedhihirisha vyakula hivyo si salama kwa afya ya binadamu. Kalonzo ameongeza…

Rais Wiliam Ruto azuru soko la hisa la Nairobi

BY  ISAYA BURUGU,11TH OCT,2022- Rais William Ruto amesema kuwa soko la hisa la Nairobi lina uwezo mkubwa kuisaidia nchi kutatua matatizo mengi yanayohusu fedha iwapo mikakati mwafaka itawekwa kuboresha utenda kazi wake. Akizungumza alipofanya ziara kwa soko hilo na kuleta Pamoja wakurugenzi…

Tume ya kitaifa ya polisi kuwahoji waliotuma maombi kwa wadhifa wa mkurugenzi wa DCI

By  Isaya Burugu,Oct 11,2022-Tume ya kitaifa ya huduma kwa polisi hivi leo inawahoji waliotuma maombi kujaza nafasi ya mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai DCI. Hatua hiyo inafuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa mkurugenzi George Kinoti.Watu kumi wametuma maombi ya kujaza nafasi…

Kanisa Katoliki lahimiza Wakenya Kuungana kuwasaidia Waathirwa wa Ukame.

Na huku Wakenya wakiendelea kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na ukame ambao umetawala kwa muda sasa kutokana na ukosefu wa mvua, maaskofu wa kanisa katoliki wametoa wito  kwa wakenya kushirikiana na kuonyesha ubinadamu kati yao kwa kutoa chakula na msaada wa…

Jimmy Wanjigi awaomba wanasiasa waliofeli katika uchaguzi kujitenga na nyadhifa za utmishi wa umma.

Mfanyibiashara Jimmy Wanjigi amewaomba wanasiasa walioshindwa katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, kutotumia nyadhifa za utumishi wa umma kurejea uongozini na badala yake kuwaruhusu wakenya wengine waliohitimu kutwaa nyadhifa hizo. Wanjigi ambaye alizungumza katika Kaunti ya Migori  siku ya Jumapili 10.Oktoba 2022,…