Kesi ya ufisadi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu yatupiliwa mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Aliyekuwa gavana wa kiambu Ferdinand Waititu amepata afueni baada ya mahakama kutupilia mbali kesi ya ufisadi iliyokuwa ikimkabili kutokana na ukosefu wa ushahidi wa kutosha. Waititu alikuwa ameshtakiwa pamoja na wenzake 12 kwa kupanga njama ya kutoa zabuni ya barabara ya shilingi…

Serikali ya Narok yaahidi kujenga kiwanda cha maziwa ili kuwawezesha wakaazi wa kaunti hiyo haswa wafugaji.

Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu ameahidi kufanya ujenzi wa kiwanda cha maziwa katika kaunti ya Narok kwa lengo la kuwawezesha wananchi wa Narok na hasa wafugaji kunufaika na maziwa ya mifugo wao. Ntutu akizungumza katika eneo la Sikinani Narok…

Wakili Paul Gicheru anazikwa hivi leo katika Kijiji cha weda Kabatini eneo bunge la Bahati kaunti ya Nakuru.

Wakili Paul Gicheru anazikwa hivi leo katika Kijiji cha weda Kabatini eneo bunge la Bahati kaunti ya Nakuru. Gicheru alikuwa anatuhumiwa na mahakama ya ICC kuwahonga mashahidi katika kesi iliyokuwa ikimkumba rais Wiliam Ruto na mwanahabari Joshua Sang .Paul Gicheru alifariki mwezi…

Mbunge wa Sirisia John Waluke kutumikia kifungo chake cha miaka 67 gerezani baada ya mahakama kuu kutupilia mbali rufaa yake.

  Mahakama kuu imetupilia mbali rufaa ya mbunge wa Sirisia John Waluke  sasa hiyo ikiwa na maana kuwa mbunge huyo atahitajika  kutumikia kifungo chake cha miaka 67. Kifungo hicho alikuwa amepewa na mahakama ya chini.Jaji Esther Maina wa mahakama kuu amesema kuwa…

Rais William Ruto aelekea nchini Ethiopia kwa mazungumzo na waziri mkuu wa taifa hilo Abiy Ahmed

Rais Wiliam Ruto ameondoka nchini leo kuelekea nchini Ethiopia ambapo amepangiwa kukutana na Waziri mkuu wa taifa hilo Abiy Ahmed Ali.Viongozi hao wawili watakuwa na mazungumzo ya Pamoja kuhusu kuboresha uchumui na mazingira ya kuendesha biashara kati ya nchi hizi mbili.Baadaye wataongoza…

TSC yaajiri waalimu 14,460 kusaidia kutatua uhaba wa waalimu nchini.

Dkt. Macharia aidha amempongeza Rais William Ruto kwa kujitolea kuimarisha sekta ya elimu nchini, na hasa kwa uamuzi wake wa kuunda jopokazi litakalosaidia katika kuangazia ufaafu na jinsi mfumo mpya wa elimu wa CBC unatekelezwa.

Gavana Ann Waiguru apona baada ya Wangui Ngirici kuondoa kesi ya kupinga ushindi wake.

Aliyekuwa Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kirinyaga katika uchaguzi wa Agosti 9 Wangui Ngirici, ameondoa kesi aliyowasilisha mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Anne Waiguru. Katika taarifa yake kutangaza uamuzi huo, mwanasiasa huyo amesema aliafikia uamuzi huo baada ya kuichunguza…

Wakaazi wa mpakani waendelea kuwa na wasiwasi kutokana na uwezekano wa virusi vya ebola kuingia humu nchini

Wakaazi wa mpakani wameendelea kuwa na wasiwasi kutokana na uwezekano wa virusi vya ebola kuingia humu nchini.Wakizungumza na waandishi wa habari,wakaazi hao wamesema kuwa wana hofu ikizingatiwa kwamba baadhi ya wakaazi wa Uganda bado wanaingia nchini.Aidha naibu kaunti kamishna wa Busia Kipchumba…