Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah aibua shutuma dhidi ya aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta.

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah ameibua shutuma dhidi ya aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta akidai kuwa yeye ndiye aliyesababisha mgawanyiko wa viongozi kuhusu ripoti ya mazungumzo ya kitaifa. Hii ni baada ya aliyekuwa mgombea mwenza wa urais wa Azimio…

Kesi yawasilishwa mahakamani kupinga matokeo ya KCPE yaliyotolewa wiki jana.

Kesi imewasilishwa mahakamani kupinga matokeo ya KCPE yaliyotolewa na Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) wiki jana. Katika kesi hiyo, wazazi wa mwanafunzi kutoka shule ya Set Green Hill Academy iliyoko Kisii, wanaitaka mahakama kuzuia KNEC kuanza zoezi la usajili wa kidato…

KNEC yaahidi kurekebisha baadhi ya makosa yaliyoripotiwa na baadhi ya watahiniwa.

Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini (KNEC) limezungumzia baadhi ya hitilafu zilizoripotiwa na baadhi ya watahiniwa katika matokeo ya hivi punde ya KCPE 2023. Baraza hilo katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari siku ya Jumamosi lilibainisha kuwa limepokea malalamishi kufuatia baadhi…

Maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wawakamata wafanyikazi wanne wa Wells Fargo wanaoaminika kusaidia katika wizi wa zaidi ya shilingi milioni Ksh.94 wa Quickmart

BY ISAYA BURUGU 25TH NOV 2023-Maafisa wa upelelezi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wamewakamata wafanyikazi wanne wa Wells Fargo wanaoaminika kusaidia katika wizi wa zaidi ya shilingi milioni Ksh.94 wa Quickmart uliotokea wiki mbili zilizopita. kukamatwa kwa wanne hao ,…

KDF kutumia helikopta zao kusambaza msaada sehemu zilizoathiriwa na mafuriko ya El Nino-Ruto.

BY ISAYA BURUGU,25TH NOV 2023-Rais William Ruto amewaamuru Wanajeshi wa Ulinzi wa Kenya (KDF) kutumia helikopta zao kusambaza bidhaa muhimu kama vile chakula na dawa katika maeneo ya nchi yaliyoathiriwa na mafuriko ya El Nino. Akizungumza hivi leo katika Ikulu ya Nairobi…

jumuiya

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Wapokea Taifa la Somalia kama Mwanachama.

 Viongozi wa Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamepokea kwa furaha taifa la Somalia kama mwanachama wa nane. Hatua hii rasmi ilitangazwa rasmi wakati wa Kikao cha 23 cha Marais kilichofanyika mjini Arusha, Tanzania, ambapo marais na wakuu wa mataifa wanachama walijumuika.…

Mvua kubwa yatarajiwa kuendelea kunyesha katika maeneo mengi ya nchi.

Mvua kubwa inatarajiwa kuendelea kunyesha katika maeneo mengi ya nchi, kulingana na utabiri wa kila wiki wa Idara ya Hali ya Hewa nchini. Kulingana na mtaalamu wa hali ya hewa, dhoruba huenda zikatokea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za Juu Mashariki…

Rais Ruto atoa wito wa kubuniwa kwa hatua endelevu na bunifu katika kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi

BY ISAYA BURUGU,24TH NOV,2023-Rais William Ruto amesema ni sharti hatua za kiubunifu na endelevu zibuniwe ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.Hatua hizi, alibainisha, zitachukuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati ikielekea Dubai kwa COP28 baadaye mwezi huu. Akizungumza katika Kongamano…