Serikali ya Kitaifa Yazindua Mitambo ya Kidijitali Kufuatilia Miradi ya Maendeleo.

Serikali ya Kitaifa imezindua rasmi mitambo ya kidijitali inayolenga kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Chuo cha Serikali eneo la Kabete, jijini Nairobi, ukiongozwa na Katibu wa Wizara ya Usalama wa Ndani, Bwana Raymond Omollo. Mitambo hii…

Rais Wiliam Ruto alihutubia bunge la umoja wa ulaya,ataka ulaya kuunga mkono Kenya katika mpango wa Haiti

BY ISAYA BURUGU,21ST NOV,2023-Rais Wiliam Ruto hivi leo amelihutubia bunge la umoja wa ulaya jijini Strathburg nchini Ufaranza. Rais Ruto amesisitiza kujitolea kwa Kenya,katika kufanya kazi na mataiafa ya bara ulaya ili kuboresha uhusiano wakibiashara zilizo muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kibiashara…

Kaunti ya Mombasa yaorodheshwa kama kaunti ambayo ina visa vingi vya unyakuzi wa ardhi nchini.

Kaunti ya Mombasa imeorodheshwa kama kaunti ambayo ina visa vingi vya unyakuzi wa ardhi nchini. Haya ni kwa mujibu wa Tume ya maadili na kupambana na Ufisadi nchini EACC. Hata hivyo tume hiyo imefanikiwa kurejesha Vipande vitatu vya Ardhi vilivyokuwa vimenyakuliwa kutoka…

Mwalimu aaga dunia Garissa

Mtahini wa KCSE Afariki baada ya Kugongwa na Kipanga cha Helikopta, Garissa.

Mwalimu mmoja katika kaunti ya Garissa ameaga dunia asubuhi ya Jumanne, baada ya kugongwa kichwani na kipanga (Propeller) ya helikopta iliyokuwa ikisafirisha mtihani wa KCSE. Tukio hilo limetokea eneo la Masalani huko Ijara, wakati wa usamabazaji wa mitihani katika vituo mbalimbali. Kamishna…

Mahakama yatoa uamuzi kusitisha agizo la serikali kutaka maafisa 67 wa polisi kusimamishwa kazi

BY ISAYA BURUGU,20TH NOV,2023-Mahakama Kuu imetoa uamuzi wa kusitisha agizo la serikali la kutaka baadhi ya maafisa wa polisi 67 kusimamishwa kazi kwa madai ya kupokea hongo na makosa mengine. Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei Alhamisi wiki jana alimwagiza Inspekta…

Aliyekuwa waziri wa hazina kuu Henry Rotich ataka mahakama kumwachilia huruArror na Kimwarer

BY ISAYA BURUGU,20TH NOV,2023-Aliyekuwa Waziri wa Hazina kuu Henry Rotich ameiomba mahakama kumwachilia huru katika kesi ya Ksh.63 bilioni ya Arror na Kimwarer, akisema kwamba simulizi kwamba pesa zilipotea au kuibiwa ni za kubuni. Anasema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi…

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga awataka mawaziri Davis Chirchir na Njuguna Ndung’u kujiuzulu.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga sasa anataka kujiuzulu mara moja kwa Waziri wa Kawi Davis Chirchir na mwenzake wa Hazina ya kitaifa Njuguna Ndung’u. Hii ni kutokana na madai ya mpango wa ununuzi wa mafuta kupitia mkataba uliotiwa saini kati ya serikali…

USALAMA

Wizara ya Usalama Yaanza Kukusanya Maoni Kuhusu Ada Mpya za Vitambulisho.

Wizara ya Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa imezindua mchakato wa kukusanya maoni kutoka kwa wananchi, kuhusu mapendekezo ya kuongeza ada za kupata nyaraka muhimu ikiwa ni pamoja na kitambulisho cha kitaifa na pasipoti. Katika taarifa iliyotolewa mapema leo na Katibu…