Chama cha UDA chaahirisha uchaguzi wa viongozi wa chama hicho uliopangwa kufanyika mwezi ujao.

Chama cha UDA kimeahirisha uchaguzi wa viongozi wa chama hicho uliopangwa kufanyika tarehe 9 Disemba 2023. Kupitia taarifa Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala amesema uchaguzi huo utafanyika Aprili 2024. Malala alibainisha kuwa zoezi hilo liliahirishwa kufuatia kikao cha Baraza la Uongozi…

Kampuni zilizotia saini mkataba wa mafuta zakanusha madai kuwa zinatumiwa kupandisha bei ya mafuta nchini.

Rais William Ruto ametetea mpango wa mafuta kati ya Serikali za Kenya, Saudi Arabia na UAE akisema uliendeshwa kwa uwazi. Kwa mujibu wa rais Ruto ni kwamba mpango huo ulikuwa muhimu katika kupunguza shinikizo la Dola huku akidai kuwa ukosefu wa sarafu…

Wambui Nyutu NCIC

NCIC Yaeleza Ongezeko la Uajiri wa Kikabila katika Serikali za Kaunti Nchini

Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) imetoa ripoti inayobainisha kuongezeka kwa kiwango cha uajiri kwa misingi ya kikabila katika serikali za kaunti nchini. Ripoti hiyo inasisitiza kuwa hali hii imeongezeka, hasa katika serikali za kaunti zilizoingia madarakani mwaka jana, ikilinganishwa…

Mshukiwa Mkuu wa Ujambazi North Rift akamatwa

Mshukiwa Mkuu wa Wizi wa Mifugo Kaskazini Mwa Rift Valley Atiwa Nguvuni.

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Baringo wamefanikiwa kumtia nguvuni mshukiwa mkuu wa wizi wa mifugo na ujambazi katika maeneo ya Kaskazini mwa Bonde la Ufa. Mshukiwa huyo, Lonyangapat Amerinyang, alikamatwa mchana wa Alhamisi katika eneo la Kapedo Akoret, Kaunti Ndogo ya…

Serikali yatakiwa kuweka wazi mkataba wa ununuzi wa mafuta uliotiwa saini kati ya Kenya, Saudi Arabia na UAE.

Kinara wa Azimio la umoja Raila Odinga ameitaka serikali kuweka wazi mkataba wa ununuzi wa mafuta uliotiwa saini kati ya Kenya, Saudi Arabia na UAE akitaja ulaghai na ufisadi kwenye mkataba huo. Kwenye kikao na waandishi wa habari, Odinga amesema kuwa mkataba…

Bunge la kitaifa laidhinisha mchakato wa kutumwa kwa maafisa 1000 wa polisi nchini Haiti.

Bunge la kitaifa limeidhinisha mchakato wa kutumwa kwa maafisa 1000 wa polisi nchini Haiti, chini ya ujumbe wa kulinda amani ulioidhinisha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN). Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Idara ya Utawala na Usalama wa Ndani…

Rais William Ruto asema atafanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Mawaziri, Makatibu Wakuu, na Baraza la Washauri wamekusanyika katika Kituo cha Mikutano cha Edge huko South C jijini Nairobi, kwa mkutano wa siku mbili. Mkutano huo unatumika kutafakari mwaka wa kwanza wa Kenya Kwanza madarakani huku kukiwa na wasiwasi kuhusu kupanda kwa…

Polisi katika kaunti ya Baringo wamkamata mshukiwa mkuu wa ujambazi huko Kapedo.

Polisi katika kaunti ya Baringo wamemkamata mshukiwa wa ujambazi huko Kapedo Akoret, Kaunti Ndogo ya Tiaty na kupata bunduki mbili na risasi 15. Kulingana na polisi katika eneo hilo, Lonyangapat Amerinyang’ amekuwa akifuatiliwa na polisi kwa miaka minne iliyopita na wanashuku kuwa…