Msemaji wa serikali Isaac Mwaura atetea safari za Rais William Ruto nje ya nchi.

Msemaji wa serikali Isaac Mwaura ametetea safari za Rais William Ruto nje ya nchi. Akihutubia wanahabari alipokuwa akielezea mafanikio ya serikali, Mwaura alisema Kenya imepata manufaa ya thamani ya Ksh.2 trilioni kutokana na mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo Ruto ametia saini tangu…

KAA Yatangaza Mipango Ya Ukarabati wa Miundombinu JKIA.

Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini (KAA) imetangaza kwamba imeanzisha juhudi za kuboresha na kurekebisha miundo mbinu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi. Kulingana na taarifa iliyotolewa na KAA siku ya Jumatano, matatizo ya…

Mvua zinazoendelea kunyesha zitashuhudiwa katika muda wa wiki moja ijayo.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini imesema kuwa mvua zinazoendelea kunyesha zitashuhudiwa katika muda wa wiki moja ijayo ambapo walioathiriwa na mafuriko huenda wakaathirika Zaidi kutokana na mvua hizo. Katika taarifa ya kila wiki ya hali ya hewa, mkurugenzi wa…

Romania President in Kenya

Rais William Ruto Ampokea Rais Klaus Iohannis wa Romania kwa Ziara Rasmi

Kiongozi wa Taifa Rais William Ruto amekutana na Rais wa Romania, Klaus Iohannis, ambaye alifika nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu. Rais Iohannis na mkewe Carmen Johannis walipokelewa kwa heshima kubwa katika Ikulu ya Nairobi na Rais Ruto, Mama wa Taifa…

Serikali Za Kaunti Zatakiwa Kuajiri Wahudumu Zaidi Wa Afya

BY ISAYA BURUGU,13TH NOV,2023-KATIBU katika Wizara ya Afya Mary Muthoni amehimiza magavana kuajiri wahudumu zaidi wa afya zaidi ili kupunguza uhaba unaoshuhudiwa katika vituo vya afya nchini. Kulingana na Bi Muthoni, uchunguzi wa serikali ya kitaifa unaonyesha kuwa hospitali nyingi zina wafanyikazi…

Kinara wa Azimio la umoja One Kenya Raila Odinga amtaka rais Ruto kusaka mbinu zingine za kupata fedha wala sio ushuru

BY ISAYA BURUGU,13TH NOV,2023-Kiongozi wa Chama cha Azimio La Umoja One Kenya Raila Odinga ametoa changamoto kwa Rais William Ruto kutafuta njia mbadala za kupata mapato ya maendeleo nchini badala ya kuwatoza Wakenya ushuru mkubwa. Odinga alimshutumu Rais Ruto kwa kuwakatisha tamaa…

KNEC yawaonya watahiniwa wa KCSE kuwa waangalifu dhidi ya karatasi ghushi za mtihani.

Baraza la Kitaifa la Mitihani humu nchini (KNEC) limewaonya watahiniwa wanaofanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE) kuwa waangalifu dhidi ya karatasi ghushi za mtihani zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii. Afisa Mkuu Mtendaji wa KNEC Dkt. David Njengere amethibitisha…

Viongozi mbalimbali kutoka pembe zote za taifa hii leo waongoza zoezi la upanzi wa miti.

Viongozi mbalimbali kutoka pembe zote za taifa hii leo wameongoza zoezi la upanzi wa miti, ambalo limeendeshwa katika sehemu mbalimbali nchini. Viongozi wakuu serikalini wakiongozwa na Rais William Ruto na mawaziri wote nchini wamepanda miti katika kaunti mbalimbali huku wakimpongeza rais Ruto…