Rais William Ruto aliongoza taifa kwenye sherehe za siku ya mashujaa katika uga wa Green Stadium mjini Kericho.

Rais William Ruto hii leo ameliongoza taifa kwenye sherehe za siku ya mashujaa ambazo ziliandaliwa katika uga wa Green Stadium mjini Kericho. Wakati wa sherehe hizo rais Ruto amezindua mpango wa afya kwa wote UHC ambapo shehena za dawa zilitumwa kwa kauti…

Maandalizi ya Mashujaa

Maandalizi ya Maadhimisho ya Mashujaa Yamekamilika Katika Kaunti ya Kericho.

Matayarisho ya maadhimisho ya sherehe za kitaifa za Mashujaa katika Kaunti ya Kericho yamekamilika, tayari kwa hafla kubwa itakayofanyika siku ya Ijumaa ya tarehe 20. Oktoba 2023. Kilele cha maandalizi haya kilishuhudia mwanakandarasi aliyepewa jukumu la ukarabati wa Uwanja wa Kericho Green…

Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) imethibitisha kujiuzulu kwa Mkurugenzi Mkuu aliyesimamishwa kwa muda Ezra Chiloba .

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) imethibitisha kujiuzulu kwa Mkurugenzi Mkuu aliyesimamishwa kwa muda Ezra Chiloba . Bodi hiyo ilisema katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba Chiloba alijiuzulu siku ya Jumatano, Oktoba 18 katika barua kwa mwenyekiti wa…

Gavana wa Kaunti ya Narok Patric Ntutu azindua kituo cha kusaidia katika ukusanyaji wa ushuru mjini Narok.

Gavana wa Kaunti ya Narok Patric Ntutu, mapema leo amezindua kituo cha kusaidia katika ukusanyaji wa ushuru mjini Narok, kituo ambacho kitawasaidia wananchi wa kaunti hii katika utekelezaji wa jukumu lao la kulipa ushuru. Akizungumza katika kituo hicho, gavana Ntutu amesema kwamba…

Waziri wa masuala ya kigeni Musalia Mudavadi aahidi kuwalinda wakenya wanaoishi ughaibuni.

Mkuu wa Mawaziri na ambaye pia ni Waziri wa Masuala ya Kigeni, Musalia Mudavadi amesema kuwa serikali itahakikisha wakenya wanaoishi nje ya nchi hawadhalilishwi katika mataifa hayo ya kigeni. Mudavadi amesema Kenya haitalegea katika juhudi zake za kuwalinda watu wake popote walipo…

kamati ya mazungumzo

Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo ya Pande Mbili Yaongezewa siku 30 zaidi.

Bunge la taifa limeongeza muda wa kuhudumu wa Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo ya Pande Mbili kwa siku 30 zaidi. Kamati hiyo inayoongozwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Taifa, Kimani Ichungwa, na Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka, itaendelea na majadiliano…

Moses Kuria

Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria Atangaza Kukabiliana na Wazembe Kazini.

Waziri wa Utumishi wa Umma, Moses Kuria, ametoa ilani kali kwa maafisa wa umma wanaozembea katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Taarifa hii imetolewa wakati wa kikao cha waandishi wa habari kilichofanyika baada yake kupokea nyaraka za ofisi hiyo kutoka kwa mtangulizi…

Naibu wa rais rigathi Gachagua azindua rasmi kongamano la afya la siku nne.

Naibu wa rais rigathi Gachagua amezindua rasmi kongamano la afya la siku nne litakalowaleta pamoja wadau wa afya huku mpango wa Afya kwa wote UHC ukitarajiwa kuzinduliwa siku ya Maadhimisho ya Mashujaa tarehe 20 mwezi huu. Akizungumza baada ya kuzindua kongamano hilo…