Serikali yapunguza bajeti ya jumla ya mwaka huu wa kifedha kwa KSh132.46 bilioni.

Serikali imepunguza bajeti ya jumla ya mwaka huu wa kifedha kwa KSh132.46 bilioni kutoka KSh3.981 trilioni hadi KSh3.848 trilioni. Hili ni punguzo la asilimia 3.3. Tangazo hili lilitolewa wakati Rais William Ruto alipotia saini kuwa sheria Mswada wa bajeti ya ziada wa…

Jeshi la Wanahewa

Rais Ruto Kuongoza Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wanahewa.

Rais William Ruto leo anatarajiwa kuongoza hafla ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Wanahewa la Kenya. Sherehe hizi zinatarajiwa kufanyika katika kambi ya Moi Airbase, Eastleigh, jijini Nairobi. Kiongozi wa taifa, ambaye amekuwa katika ziara ya kikazi nchini Korea Kusini,…

Mahakama yaondoa kesi ya jinai dhidi ya Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na washtakiwa wengine sita.

Mahakama ya Nairobi imeondoa kesi ya jinai dhidi ya Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na washtakiwa wengine sita. Hii ni baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) kutuma maombi ya kutaka kesi hiyo iondolewe, baada ya uamuzi wa mahakama kuu…

Serikali yaahidi kuendelea kumpigia debe Raila Odinga kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti wa AU.

Serikali ya Kenya imeahidi kuendelea kumpigia debe kinara wa azimio la umoja Raila Odinga kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti wa muungano wa umoja wa Afrika huku uchaguzi ukiratibiwa kufanyika mwezi Februari mwaka ujao. Haya yamewekwa wazi na mkuu wa baraza la mawaziri nchini…

Dorcas Rigathi

Vijana Wahimizwa Kushiriki Katika Mafunzo Kuhusu Afya ya Akili.

Mke wa Naibu Rais Pst. Dorcas Rigathi ameendelea kusisitiza azma yake ya kuwasaidia vijana katika kupambana na changamoto za uraibu wa dawa za kulevya na kusimama kidete katika kutetea maslahi yao, hususan vijana wa kiume nchini. Haya yalijitokeza baada ya kuhudhuria na…

Takriban familia 40,000 zahama kwa hiari kutoka kwa hifadhi za mito.

Takriban familia 40,000 zinazojumuisha watu 181,000 zimehama kwa hiari kutoka kwa hifadhi za mito ya Nairobi, Mathare na Ngong na vijito vingine vidogo vya mfumo wa Ikolojia wa Mito ya Nairobi. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa usalama wa ndani Kithure…

Ripoti ya Makadirio ya Akaunti ya wizara ya Afya ya kitaifa yazinduliwa.

Katibu Mkuu wa Huduma za Matibabu kwenye wizara ya afya Harry Kimtai, alizindua rasmi Ripoti ya Makadirio ya Akaunti ya wizara ya Afya ya Kitaifa kwa mwaka kifedha 2019/20 hadi 2021/22. Ripoti hiyo inasisitiza dhamira ya serikali ya upatikanaji wa huduma za…

sIKU YA uTAMADUNI

Kenya Kuungana na Ulimwengu Kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Utamaduni.

Siku ya leo, Kenya inaungana na mataifa mengine kote ulimwenguni katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utamaduni na Tofauti za Kijamii. Maadhimisho haya, ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 21 Mei tangu mwaka wa 2005, yananuia kusherehekea utofauti wa kijamii na kuimarisha…