Waziri Aden Duale akihutubia Maseneta

Waziri Duale Asema Jeshi la KDF litaondoka Somalia Mwisho wa Mwaka 2024.

Waziri wa Ulinzi Aden Duale amejiwasilisha mbele ya Bunge la Seneti asubuhi ya siku ya Jumatano, ili kujibu maswali mbalimbali kuhusu utendakazi wa Wizara yake. Katika kikao hicho, maseneta walipata nafasi ya kuuliza maswali kuhusu Idara ya Ulinzi wa Taifa, na kwa…

Seneta mteule Gloria Orwoba aruhusiwa kwa muda kurejea katika Seneti

BY ISAYA BURUGU,3RD OCT,2023-Seneta mteule Gloria Orwoba ameruhusiwa kwa muda kurejea katika Seneti baada ya kupokea maagizo kutoka kwa mahakama ya kuzuia Seneti kumsimamisha kazi. Orwoba, ambaye alikuwa amesimamishwa kazi na Seneti kwa muda wa miezi sita, alipata maagizo kutoka kwa Jaji…

Mashirika ya kiserikali  yaagizwa kupunguza matumizi yao kwa asilimia 10 katika mwaka huu wa fedha

BY ISAYA BURUGU,3RD OCT,2023-Mashirika ya kiserikali  yameagizwa kupunguza matumizi yao kwa asilimia 10 katika mwaka huu wa fedha ili kuwianisha matumizi yao na rasilimali zilizopo. Rais William Ruto alitoa maagizo hayo kama sehemu ya hatua za kubana matumizi ili kuhakikisha mashirika ya…

EACC yapendekeza kuajiriwa kwa wafanyakazi Zaidi ili kumaliza mrundiko wa kesi za ufisadi.

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC hii leo imefika mbele ya kamati ya mazungumzo ya maridhiano kati ya Kenya kwanza na Azimio ili kuwasilisha mapendekezo yao. Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt. David Oginde alipendekeza tume hiyo kuongezewa wafanyakazi Zaidi…

Maaskofu wa KCCB wawasilisha mapendekezo.

Mazungumzo Ya Kitaifa | KCCB Yapendekeza Kufanyika Kwa Mabadiliko ya Katiba.

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini KCCB, limeeleza kwamba kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko ya katiba nchini. Haya yaliwekwa wazi katika mapendekezo mbele ya kamati ya mazungumzo ya kitaifa katika ukumbi wa Bomas siku ya Jumanne. Maaskofu katika ujumbe wao wameeleza…

mkurugenzi wa Lesedi Developers Limited, Geoffrey Kiragu, aachiliwa kwa bondi ya Ksh.5 milioni na mdhamini wa kiasi sawa na hicho

BY ISAYA BURUGU,2ND OCT 2023-Mahakama ya Thika imemwachilia mkurugenzi aliyehasimiana wa Lesedi Developers Limited, Geoffrey Kiragu, kwa bondi ya Ksh.5 milioni na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au dhamana mbadala ya Ksh.5 milioni pesa taslimu. Akiwa amefikishwa mbele ya Hakimu Mkuu…

Gavana Waiguru aahidi kupigania maslahi ya kaunti zote katika muhula wake wa pili kama mwenyekiti wa magavana

BY ISAYA BURUGU,2ND OCT 2023-Gavana wa Kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Magavana kuhudumu kwa muhula wa pili.Waiguru alichaguliwa kwa muhula wa pili afisini kupitia makubaliano ya jumla wakati wa mkutano kamili wa baraza uliofanyika Nairobi.Wakati huo…

Shughuli za uchukuzi zatatizika kwenye barabara kuu ya Mai mahiu-Narok wakaazi wa duka moja wakiandamana kulalamikia utovu wa usalama

BY ISAYA BURUGU,2ND OCT,2023-Shughuli za usafiri zimetatizika  kwa muda mchana wa leo baada ya wananchi waliojawa ghadhabu kuandamana na kufunga bara bara kuu ya Narok-Mai Mahiu eneo la Duka moja kwenye kaunti ndogo ya Narok mashariki kulalamikia kile walichodai kuwa ongezeko la…