DPP MPYA: Renson Mulele Aapishwa Kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

Renson Mulele Ingonga sasa ndiye mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya Umma (DPP), baada yake kuapishwa asubuhi ya leo kutwaa wadhifa huu rasmi, katika hafla iliyoandaliwa kwenye ikulu ya Nairobi na kushuhudiwa na Rais William Ruto pamoja na wakuu wengine wa serikali na…

Wawili wakamatwa Embu na Pembe za Ndovu zenye Dhamani ya Milioni 10.

Idara ya Huduma za Polisi nchini (NPS) kwa ushirikiano na Maafisa wa Wanyamapori wa Kenya (KWS) wamefanikiwa kuwatia nguvuni washukiwa wawili waliokuwa na pembe mbili za ndovu katika Kaunti ya Embu. Kulingana na taarifa kutoka NPS, washukiwa hao walikamatwa siku ya Ijumaa…

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki apiga marufuku mikutano ya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza maarufu okolea.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki amepiga marufuku mikutano ya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza chini ya mpango wake wa kuwafikia watu kwa jina Okolea. Agizo hilo linakuja baada ya fujo kushuhudiwa Jumapili iliyopita wakati wa hafla ya Mwangaza ya ‘Mpango…

Malala UDA

Mambo Yote Shwari Ndani ya UDA, Cleophas Malala Akanusha Semi Kuhusu Mvutano.

Katibu wa Kitaifa wa Chama tawala cha UDA, Cleophas Malala, amekanusha uvumi wa kuwepo nyufa ndani ya chama hicho. Akizungumza wakati wa ziara yake ya ufunguzi wa ofisi za chama mjini Narok siku ya Ijumaa, Malala amesisitIza kuwa hakuna chochote kinachowababaisha katika…

Amri yatolewa ya kuwaua wahalifu wowote wanaolenga maafisa wa usalama au kambi za usalama.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ametoa amri ya kuwaua wahalifu wowote wanaolenga maafisa wa usalama au kambi za usalama. Akizungumza alipokuwa akizindua kambi ya GSU katika Eneo Bunge la Tiaty, Kaunti ya Baringo, Kindiki alisema mhalifu yeyote atakaye mpiga risasi…

Mahakama ya Mizozo ya Vyama vya Kisiasa yaongeza muda wa agizo la kukizuia chama cha ODM kuwatimua wabunge watano.

Mahakama ya Mizozo ya Vyama vya Kisiasa imeongeza muda wa agizo la kukizuia chama cha ODM kuwatimua Seneta wa Kisumu Tom Ojienda na wabunge Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o na Elisha Odhiambo kutoka kwa chama hicho. Mahakama hiyo pia iliagiza kesi hiyo itajwe…

Olposimoru

Baba Katili Amwangamiza Mwanawe wa miaka 12 Kwa Panga Olposimoru, Narok.

Maafisa wa polisi katika kituo cha Olposimoru, Narok Kaskazini, wamemkamata mwanaume mmoja kwa tuhuma za kumwua mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 12 katika kijiji cha Kipendeni eneo la Olengape. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maafisa wa Idara ya Upelelezi…

Jeremiah Kioni bado aaminika kuwa Katibu Mkuu halali wa chama cha Jubilee kulingana na utafiti uliofanya na TIFA.

Jeremiah Kioni bado anaaminika kuwa Katibu Mkuu halali wa chama cha Jubilee kulingana na utafiti uliofanya na TIFA. Katika utafiti huo uliotolewa leo Alhamisi, asilimia 32% ya waliohojiwa wanamtambua Kioni kama katibu mkuu wa Jubilee huku 21% wakimchukulia Kega kama katibu mkuu…