Fisi awavamia wananchi Naikarra

Watu 4 Waachwa na Majeraha Baada ya Kushambuliwa na Fisi – Naikarra, Narok.

Watu wanne wa familia moja katika kijiji cha Olopilukunya, eneo la Naikarra katika kaunti ndogo ya Narok magharibi, wanauguza majeraha mabaya baada ya kuvamiwa na fisi usiku wa kuamkia leo. Jackson Masago, ambaye ni mmoja wa jamaa wa familia hiyo, ameeleza kuwa…

Wanafunzi wawili wa chuo kikuu cha Maasai wazama katika mto Enkare mjini Narok.

Shughuli ya kuiopoa miili ya wanafunzi wawili wa chuo kikuu cha Maasai Mara inaendelea katika mto wa Enkare Narok. Akiongoza Shughuli hiyo ya uopozi, kamishana wa kaunti ya Narok Rueben Lotiatia amesema wawili hao walikuwa wakiuvuka mto huo ambapo mmoja wao aliteleza…

Ajali

Watu 6 Waangamia Kwenye Ajali ya Barabara Eneo la Silanga, Narok

Watu sita wameaga dunia na wengine saba kujeruhiwa vibaya katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea eneo la Silanga kwenye barabara kuu ya Narok kuelekea Mulot. Ajali hiyo imetokea saa tatu usiku siku ya Jumapili na imehusisha magari mawili, gari aina ya Toyota…

OGOLLA

Mkuu wa Majeshi Jenerali Francis Ogolla Kuzikwa Siku ya Jumapili Familia Yasema.

Aliyekuwa Mkuu wa majeshi humu nchini Marehemu Jenerali Francis Ogolla, ambaye alifariki katika ajali ya ndege katika kaunti ya Elgeiyo Marakwet, atazikwa Jumapili ya tarehe 21 mwezi wa Aprili nyumbani kwake katika eneo la Alego Usonga, Kaunti ya Siaya. Kulingana na taarifa…

Askofu mkuu Maurice Muhatia ateuliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la maaskofu KCCB.

Askofu mkuu wa jimbo kuu la Kisumu Maurice Muhatia Makumba ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki KCCB kwa muda wa miaka tatu ijayo. Askofu mkuu Muhatia, anachukua nafasi hii kutoka kwa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Mombasa…

KUTRRH

Hospitali ya KUTRRH Yaajiri Madaktari Wa Kigeni Kuwatibu Wagonjwa wa Saratani.

Hospitali ya Rufaa, Mafunzo na Utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH) imetangaza hatua ya kuwaajiri madaktari watano wa kigeni ili kuongeza uwezo wa kutoa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa. Hatua hii inakuja wakati ambapo matabibu nchini wanashiriki mgomo, ambao umeingia…

Maandamano ya Madaktari

Madaktari Kushiriki Maandamano ya Amani Jumanne kushinikiza Utekelezaji wa CBA

Muungano wa Madaktari nchini, KMPDU, umetangaza mipango ya kuandaa maandamano ya amani siku ya Jumanne ijayo, lengo likiwa ni kuendelea kuisukuma serikali kusikiliza kilio chao. Katibu Mkuu wa KMPDU, Davji Atellah, kupitia barua aliyoituma kwa Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nairobi,…

Mgomo wa madaktari waingia siku ya 22 leo hii.

Muungano wa madaktari nchini KMPDU umeendelea kumkashifu waziri wa afya Susan Nakuhmicha kwa kupendekeza kupunguzwa kwa mishahara ya madaktari wanagenzi kinyume na ilivyoainishwa kwenye mkataba wa maelewano wa mwaka 2017. Wakiwahutubia waandishi wa habari jijini Nairobi,muungano huo umeeleza kuwa mshahara ambao wanagenzi…