Rais William Ruto asisitiza kwamba hatakubali kugawana nyadhifa za uongozi na upinzani.

Rais William Ruto amesisitiza msimamo wake kwamba hatakubali kugawana nyadhifa za uongozi na upinzani kwa njia yoyote ile. Akiwahutubia wananchi katika eneo la Githurai kaunti ya Kiambu baada ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo, Rais amesema kwamba hatakubali kuyumbishwa na vitiso vya…

Narok-og_image

Mahakama ya Narok Yawaachilia kwa Dhamana Wazazi Waliomlazimisha Binti Yao Mjamzito Kukeketwa.

Mahakama ya Narok imewaachilia kwa dhamana wazazi wa msichana mmoja mwenye umri wa miaka 15, baada yao kumlazimisha kukeketwa kinyume cha sheria licha ya kuwa mjamzito. Wazazi hao, Dennis Kishoiyan na mkewe Mariciana Kishoyian, walifikishwa mbele ya mahakama ya Narok siku ya…

NTSA-CARS

NTSA Yaonya Madereva Dhidi ya Utovu wa Nidhamu Shule Zikifungwa.

Huku shule zikielekea kufungwa juma lijalo, Mamlaka ya Trafiki na Usalama Barabarani (NTSA) imechukua hatua za tahadhari kwa madereva na wachukuzi wengine wa umma dhidi ya kuvunja sheria za trafiki na utovu wa nidhamu barabarani. Hatua hii inalenga kuhakikisha usalama wa wanafunzi…

Amnesty International yafichua kuwa watu 11 walipoteza maisha wakati wa maandamano.

Ripoti mpya ya Amnesty International imefichua kuwa takriban watu 11 walipoteza maisha katika kaunti za Kisumu na Kisii wakati wa maandamano dhidi ya serikali majuma mawili yaliyopita. Matokeo kutoka kwa ripoti hiyo, iliyotolewa kwa pamoja na Chama cha mawakili LSK na Chama…

Serikali ya kaunti ya Kisii kusambaza matenki ya maji mashuleni

BY ISAYA BURUGU 4TH AUG 2023-Serikali ya kaunti ya Kisii imeanza mpango wa kusambaza matenki ya maji   katika shule  zinazokumbwa na changamoto za kupata maji. Vilevile mpango huo unaohusisha wizara ya maji ya kaunti hiyo unanuiwa kukabili magonjwa yanayoletwa na matumizi ya…

Rais Ruto kuanza ziara ya eneo la kati mwa nchi kesho jumamosi

BY ISAYA BURUGU 4TH AUG,2023-Rais William Ruto  ataanza ziara yakimaendeleo eneo la Mlima Kenya wikendi hii hadi wiki ijayo.Ziara hiyo ya siku tano itaanza hiyo kesho Jumamosi kwa safari ya barabarani kutoka Nairobi, ikiambatana na vituo vya kusimama Githurai na Kenol. Katika…

Serikali yadhibitisha kuwa mpango wa sarafu digitali ya World coin haujsajiliwa nchini

BY ISAYA BURUGU,3RD AUG 2023-Serikali imedhibitisha  kuwa muradi wa sarafu kidigitali ya Worldcoin, ambayo oparesheni zake zimesitishwa  humu nchini haujasajiliwa kisheria nchini Kenya. Kupitia taarifa ya Pamoja iliyotolewa na wizara za usalama wa ndani  sawa  na ile ya teknologia ya mawasiliano ya…

LSK chataka taarifa kuhusu idadi ya watu waliokamatwa wakati wa maandamano.

Chama cha mawakili nchini LSK kimewaandikia barua polisi, kutaka taarifa kuhusu idadi ya watu waliokamatwa na kuzuiliwa wakati wa maandamano ya Azimio. Pia inawataka polisi kuwapa stakabadhi zozote zinazohusiana na uchunguzi wa maiti na chanzo cha vifo vya waliofariki kutokana na maandamano…