Mtoto afariki huku watu wanane wakijeruhiwa katika ajali Nakuru

BY ISAYA BURUGU 10TH JULY 2023-Mtoto wa miaka tisa amefariki katika ajali ya barabarani usiku wa kuamkia leo katika eneo la ngata katika Barabara kuu ya Nakuru kuelekea Kisumu. Watu wengine wanane wamepata majeraha na kupelekwa hospitalini kwa matibabu. Maafisa wa polisi…

Odinga aabiri gari la uchukuzi wa umma kwenda kazini

BY ISAYA BURUGU 10TH JULY 2023-Kinara wa upinzani Raila Odinga hivi leo ameabiri gari la uchukuzi wa umma kutoka nyumbani kwake mtaani Karen hadi kazini jijini Nairobi. Raila ameungana na viongozi wengine katika safari yake hiyo ambapo ameabiri gari la umma kutoka…

Ruto Congo

Kenya na Congo Zakubaliana Kuondoa Visa kwa Usafiri Kati ya Mataifa Haya Mawili.

Serikali za Kenya na Congo zimefikia makubaliano ya kuondoa hitaji la visa ili kurahisisha usafiri kati ya mataifa hayo mawili. Muafaka huu ulitangazwa na Kiongozi wa Taifa, Rais William Ruto, ambaye yuko ziarani katika taifa la Jamhuri ya Congo, baada ya kikao…

Naibu Rais asuta zoezi la kukusanywa kwa sahihi za kumbandua rais mamlakani.

Naibu Rais Rigathi Gachagua amesuta hatua ya kinara wa Azimio Raila Odinga ya kuanzisha zoezi la kukusanya sahihi katika azma ya kumbandua mamlakani Rais William Ruto. Odinga alitangaza hatua hiyo ya kukusanya sahihi milioni 10 hapo jana wakati wa maandamano ya Saba…

Saba saba

Maandamano Ya Saba Saba | Upinzani Waanza Mchakato wa Kukusanya Sahihi.

Mrengo wa upinzani nchini unapanga kuanza mchakato wa kukusanya saini milioni 10 ifikapo mwisho wa juma lijalo, lengo likiwa ni kuwezesha kuanzishwa kwa mchakato wa kumbandua mamlakani kiongozi wa Taifa, Rais William Ruto. Hatua hii imechukuliwa baada ya kinara wa muungano wa…

DCI Yaomba Muda Zaidi Kuwazuia Waliowadhalilisha Wafanyakazi wa Kike Brown Cheese.

Idara ya DCI imeomba muda wa siku 14 zaidi ili kuandaa kesi dhidi ya washukiwa wawili wa kampuni ya Brown Cheese, wanaodaiwa kuwadhulumu wafanyakazi wa kike katika kampuni hizo, kwa kuwalazimisha kuvua nguo ili kuchunguzwa iwapo wako katika kipindi cha Hedhi. Wawili…

Baadhi ya wakaazi wa Narok wajiunga na viongozi wa Azimio la umoja kufanya mandamano.

Wakaazi wa mji wa Narok wamejiunga na viongozi wa Azimio la umoja kufanya mandamano ili kuishinikiza serikali ya Kenya Kwanza kupunguza gharama ya maisha. Wakizungumza na waandishi wa habari, wakaazi hao wameshutumu serikali ya kwa kuongeza bei ya bidhaa muhimu kama vile mafuta…

Makubaliano ya Kuimarisha Sekta ya Ukulima wa Majani Chai kuwa Sheria.

Naibu Rais Rigathi Gachagua ameahidi kwamba makubaliano yatakayofikiwa na washikadau katika sekta ya ukulima wa majani chai nchini yataidhinishwa kama sheria kupitia bunge la kitaifa na lile la seneti. Hatua hii inalenga kuboresha na kuimarisha sekta hii muhimu na kuhakikisha wakulima wanapata…