Rais William Ruto aongoza mkutano kuhusu uwekezaji barani Afrika jijini Nairobi.

Rais William Ruto hivi leo ameongoza mkutano kuhusu uwekezaji barani Afrika jijini Nairobi. Rais Ruto akizungumza kwenye mkutano huo alipendekeza bara la Afrika kuimarisha mfumo wa biashara kwa kutumia sarafu zake ili kupunguza kutegemewa kwa utumizi wa dola. Ameongeza kuwa hatua hii…

Wakaazi wa Narok wafaidika na Uchunguzi wa afya pamoja na hamasisho ya bure kuhusu saratani.

Mamia ya wakaazi mjini Narok walifaidika na Uchunguzi wa afya pamoja na hamasisho ya bure kuhusu ugonjwa wa saratani kutoka kwa wahudumu wa afya wa hospitali ya rufaa ya Narok, hospitali ya Medicatia kwa ushirikiano na kanisa la New Seventh Day Adventist.…

Seth Panyako ajiuzulu kama naibu mwenyekiti wa chama cha UDA.

Aliyekuwa naibu mwenyekiti wa chama cha UDA Seth Panyako, ameachia ngazi na kujiuzulu kutoka kwa wadhifa wake katika chama hicho. Hatua hiyo ya kujiuzulu imekujia kufuatia tofauti za misimamo ya chama na msimamo wake binafsi, huku yeye akipinga pendekezo la malipo ya…

IPOA yaanzisha uchunguzi baada ya watu sita kuuawa kwa kupigwa risasi huko Isebania.

Mamlaka Huru ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA imeanzisha uchunguzi baada ya watu sita kuuawa kwa kupigwa risasi wakati umati ulivamia Kituo cha Polisi cha Isebania huko Migori Alhamisi jioni. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi kuhusu tukio hilo, kundi hilo la…

Jamii yatakiwa kuwakumbatia wasichana badala ya kuwatenga wanapopata hedhi zao.

Huku ulimwengu ukitarajiwa kuadhimisha siku ya usafi wa hedhi duniani hapo kesho, jamii imetakiwa kuwakumbatia kina mama na wasichana badala ya kuwatenga wanapopata hedhi zao. Akizungumza na kituo hiki kwenye mahojiano ya kipekee, Afisa wa afya anayesimamia idara ya afya ya uzazi…

Kindiki

Ole wenu manabii wa uongo, Waziri Kindiki atuma onyo.

Waziri wa usalama wa ndaki Kithure kindiki ametuma onyo kali kwa wahubiri wengine wanaoendelea kuwapunja wakenya na kuwahangaisha huku wakijificha nyuma ya dini. Akizungumza katika kikao cha bunge alipojiwasilisha ili kuhojiwa na wabunge kuhusu hali ya operesheni ya uokozi katika eneo la…

Raila in Yatta

Azimio yaahidi kutumia kila njia kuishurutisha serikali kupunguza gharama ya maisha.

Kinara wa upinzani Raila Odinga amemtaka Rais William Ruto kupunguza gharama ya Maisha, na kupunguza mapendekezo yaliyo kwenye mswada wa fedha wa mwaka huu. Akizungumza katika eneo la Yatta katika kikao cha muungano wa Azimio la Umoja, Odinga aliyeambatana na viongozi wengine…

Naibu Rais Rigathi Gachagua awasuta wanaopinga asilimia 3 ya ushuru wa nyumba.

Naibu Rais Rigathi Gachagua amemtaka Rais William Ruto kutozingatia wale wanaopinga asilimia 3 ya ushuru wa nyumba. Akizungumza mjini Embu, Gachagua amesema wanaokosoa mradi huo kamwe hawatathamini ufanisi wa rais. Alidokeza kuwa miradi hiyo ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu itakomesha…