Rais William Ruto awaonya wafanyakazi wa KRA dhidi ya kuendeleza ufisadi.

Rais William Ruto amewaonya wafanyakazi wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru KRA dhidi ya kuendeleza ufisadi. Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasilisha rekodi yake ya ulipaji ushuru katika makao makuu ya KRA, rais Ruto alisema kuwa kuna baadhi ya maafisa wa KRA wanaoshirikiana…

Fulgence Kayishema

Fulgence Kayishema, Mshukiwa wa mauaji ya Kimbari nchini Rwanda, akamatwa.

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, Fulgence Kayishema, amekamatwa nchini Afrika Kusini. Haya yamesemwa Alhamisi na kitengo cha Umoja wa Mataifa cha kuchunguza uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Rwanda. Kulingana na kitengo hicho Kayishema anatuhumiwa kupanga mauaji ya karibu Watutsi elfu…

Muda wa kutotoka nje kuanzia jioni hadi alfajiri katika eneo la Chakama yaongezwa kwa siku 30

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ameongeza muda wa kutotoka nje kuanzia jioni hadi alfajiri katika eneo la Chakama Ranch kwa siku 30. Akizungumza mjini Malindi alikoenda kusimamia kuanza kwa uchunguzi wa miili 125 iliyofukuliwa katika msitu wa Shakahola Kindiki pia…

Ntutu narok

Miradi ya Maendeleo haitasimama, Gavana Ntutu awahakikishia wananchi.

Wakaazi wa kaunti ya Narok watanufaika na utengenezaji wa barabara, baada ya kuzinduliwa kwa awamu ya pili ya miradi ya maendeleo ya Kaunti. Gavana wa Kaunti ya Narok Patric Ntutu ameeleza kwamba awamu hii ya pili inaangazia miradi mingi ya ujenzi wa…

Mwanamume mmoja atoweka baada ya kuwafungia watoto wake wawili kwa minyororo.

Maafisa wa polisi katika eneo bunge la Mumias kaunti ya Kakamega wanamsaka mwanamume mwenye umri wa miaka 45 kwa jina Simon Mila Alichi ambaye aliwafungia watoto wake wawili katika chumba kimoja na kuwafunga kwa minyororo. Watoto hao walifungiwa chumbani mchana na usiku,…

Rais William Ruto aongoza zoezi la kutengeneza vitambulisho vya kidigitali.

Rais William Ruto ameongoza kongamano la ID4AFRIKA ambapo zoezi la kutengeneza vitambulisho vya kidigitali limezinduliwa. Ruto ameeleza kuwa Kenya ni miongoni mataifa ya kwanza barani Afrika kuanzisha mfumo wa sera ya ulinzi wa data unaojumuisha sheria na kanuni za data ya kibinafsi.…

Esther Ngero, katibu katika idara ya urekebishaji tabia ajiuzulu.

Katibu katika Idara ya urekebishaji wa tabia nchini Esther Ngero amejiuzulu, siku saba baada ya uhamisho wake kutoka kwa ofisi ya mkuu wa baraza la Mawaziri Musalia Mudavadi. Ngero amekua afisa wa kwanza wa serikali kujiuzulu kwa kile alichokitaja kama sababu za…

Awamu ya pili ya uzinduzi wa miradi ya CIDP, Narok yaanza rasmi.

Miradi hii ya CIPD, ni sehemu ya miradi 64 ya maendeleo itakayozinduliwa baada ya zaidi ya miradi 363 kuzinduliwa katika awamu ya kwanza