Utovu wa usalama Ololulunga:Wakuu wa usalama watakiwa kuelezea mikakati ya kukabili hali

BY  ISAYA BURUGU 6TH MAY 2023-Kufuatia visa vya uhalifu na hasa watu kuvamiwa katika eneo la Ololunga eneo bunge la Narok Kusini kaunti ya Narok katika siku za hivi karibuni,mbunge wa eneo hilo Keitalai Ole Ntutu amewataka wasimamizi wa usalama eneo hilo…

Soipan Tuya

Serikali kuzindua nambari ya simu ya bila malipo kusaidia kuwakabili wanaoharibu misitu.

Wizara ya mazingira na misitu nchini, kupitia idara ya ulinzi na uhifadhi wa misitu inapania kuzindua nambari za simu za bila malipo zitakazosaidia katika vita dhidi ya ukataji wa miti na uharibifu wa misitu katika maeneo tofauti ya taifa. Akitangaza mipango hii…

King Charles Corronation

Rais Ruto kuhudhuria hafla ya Kutawazwa kwa Mfalme Charles III wa UK siku ya Jumamosi.

Rais William Ruto ameratibiwa kuondoka nchini jioni ya leo kwa ziara rasmi barani ulaya. Kwa mujibu wa taarifa iiyochapishwa na Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed, rais ataanzia ziara yake nchini Uingereza, ambapo atajumuika na viongozi wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani kuhudhuria hafla…

Wakenya 250,000 watarajiwa kupata nafasi za ajira nchini Ujerumani.

Uhusiano mzuri kati ya Kenya na Ujerumani umeendelea kuimarika kufuatia Ziara ya Kiserikali ya Kansela Olaf Scholz siku ya Alhamisi. Katika mkutano wa pande mbili na mkutano na wanahabari katika Ikulu ya Nairobi, Rais William Ruto alitoa wito wa kupunguzwa kwa vikwazo…

Jaji Jessie Lesiit ateuliwa kuongoza tume itakayochunguza mauaji ya Shakahola.

Rais William Ruto ameunda Tume ya Uchunguzi inayojumuisha wanachama 13 kuanza uchunguzi kuhusu dhehebu la mhubiri Paul Mckenzie ambapo zaidi ya watu 100 wameripotiwa kufariki kufikia sasa. Rais Ruto, katika notisi ya gazeti la serikali iliyotolewa Ijumaa, alitaja wanachama 8 wa tume…

Watu sita waaga dunia kufuatia ajali ya barabarani Kaunti ya Homa Bay

BY ISAYA BURUGU 05,MAY 2023-Takriban watu sita wanahofiwa kufariki baada ya basi walimokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali ya barabarani karibu na Kanyadhiang, eneo bunge la Karachuonyo. Ajali hiyo imetokea wakati basi la Shule ya Sekondari ya ACK Guu lilikuwa likiwasafirisha waombolezaji kuelekea…

Upande wa mashtaka wataka siku 90 kumzuilia Paul Mackenzie

BY  ISAYA BURUGU,05,2023-Mhubiri tata Paul Mackenzie na watu wengine saba wameregeshwa mahakamani huko Shanzu hivi leo huku kesi ya mauaji inayowakumba ikiendelea.Upande wa mashtaka unaitaka mahakama kuagiza Mackenzie na watuhumiwa wengine kuzuiliwa kwa siku 90 zaidi ili kuwaruhusu polisi kukamilisha uchunguzi. Vilevile…

Mjane wa Dedan Kimathi, Mukami Kimathi aaga dunia jijini Nairobi

BY ISAYA BURUGU 05,MAY 2023-Mjane wa shujaa wa kupigania uhuru wa taifa la Kenya, Field Marshal Dedan Kimathi, Mukami Kimathi amefariki. Mama Mukami ambaye pia ni shujaa wa ukombozi wa Kenya kutoka minyororo ya ukoloni amefariki akiwa na umri wa miaka 96.…