Kindiki awaonya magaidi wanaojificha nyuma ya dini.

shughuli ya kufukua miili katika eneo la Shakahola Kaunti ya Kilifi limesitishwa hii leo kutokana na mvua kubwa katika eneo hilo, serikali sasa ikielekeza mcho yake katika shughuli za uokozi.Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amesema kwamba serikali itafanikiwa katika vita…

Luteni Jenerali Francis Omondi Ogolla ateuliwa kuwa Mkuu mpya wa Majeshi.

Rais William Ruto sasa amemteua Luteni Jenerali Francis Omondi Ogolla kuwa Mkuu mpya wa Majeshi, akichukua nafasi ya Jenerali Robert Kariuki Kibochi ambaye muda wake wa kuhudumu umefikia kikomo. Jenerali Ogolla alikuwa, akihudumu kama Makamu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi. Jenerali Kibochi,…

Rais Wiliam Ruto azindua ujenzi wa kilomita 65 za barabara mjini Ongata Rongai,atoa hakikisho bei ya unga itashuka zaidi wiki ijayo.

BY ISAYA BURUGU 28TH APRIL,2023-Rais Wiliam Ruto amesema kuwa serikali yake imejitolea kuboresha Maisha ya kila mwananchi. Akizungumza alipozindua ukarabati wa barabara ya kilomita 65 mjini Ongata Rongai,rais amesema barabara bora ndizo zitakazowawezesha wakulima kusafirisha mazao yao hadi sokoni na kupata faida.…

Maafisa wa polisi wataka kibali kumzuilia mhubiri Ezekiel Odero kwa siku 30 zaidi

BY ISAYA BURUGU,28TH APRIL,2023-Maafisa wa polisi sasa wataka kuruhusiwa kumzuilia mhubiri  Ezekiel Odero kwa siku 30 zaidi ili kukamilisha uchunguzi dhidi  yake.Mhubiri huyo awa kanisa la  New Life Prayer Centre and Church alikamatwa hiyo jana na polisi wanasema kuna Habari za kuaminika…

Sheria za kukabili pombe haramu mlima Kenya kuandaliwa kufikia mwezi Juni.

Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya washikadau wote wakiongozwa na sekta ya usalama na mahakama humu nchini ili kukomesha tishio la ugemaji, unywaji na vilevile uraibu wa pombe na dawa za kulevya katika eneo la mlima…

MCK lawakashifu polisi kwa kuwafungia nje wanahabari waliokuwa wakiripoti mkasa wa Shakahola.

Baraza la vyombo vya Habari nchini MCK limewakashifu maafisa wa polisi kwa kuwafungia nje wanahabari waliokuwa wakiripoti mkasa wa Shakahola. Katika taarifa, MCK ilisema hatua hiyo inavinyima vyombo vya habari fursa ya kuripoti kuhusu suala la maslahi ya umma.Siku ya Jumatano, wanahabari…

Rais Wiliam Ruto atia saini msuada wa ugavi wa mapato wa mwaka 2023

BY SAIAYA BURUGU 27TH APRIL,2023-Rais William Ruto ametia Saini kuwa sheria mswada wa ugavi wa mapato wa mwaka 2023 uliopitishwa na bunge la seneti wiki jana. Maseneta waliuzingatia na kupitisha msuada huo tarehe 20 mwezi huu bila marekebisho jinsi ulivyopitishwa na bunge…

Mhubiri Ezekiel Odero wa kanisa la New life akamatwa huku shughuli ya ukaguzi wa miili ya Shakahola ikianza

BY ISAYA BURUGU 27TH APRIL,2023-Shughuli ya ukaguzi wa maiti zipatazo 98 zilizopatikana kule Shakahola kaunti ya Kilifi  inatarajiwa kuanza leo katika hospitali ya Malindi.Tayari mkaguzi mkuu wa maiti wa serikali amewasili Malindi kwa zoezi hilo.Ukaguzi huo unaendeshwa ili kubaini kilichopelekea vifo hivyo.…