Chama cha Jubilee kimeagizwa kuondoka katika majengo wanayotumia kwa sasa kama makao makuu ya chama baada ya pande ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Kanini Kega na pande ya aliyekuwa Mbunge wa Ndaragwa Jeremiah Jeremiah Kioni kuzozana kuhusu uongozi wa chama hicho.
Haya yanajiri baada ya kundi linaloongozwa na mbunge Kega kuonekana wakirusha mawe na vitu vingine kwenye jumba hilo baada ya kukataliwa kuingia.
Mbunge Kega aliungana na Mbunge Mteule Sabina Chege na Mbunge wa Eldas Adan Keynan, miongoni mwa wengine.
Taarifa iliyofuata kutoka kwa mmiliki wa mali hiyo iliamuru wahusika kuondoka katika eneo hilo kwa madai kuwa wamekiuka masharti ya upangaji.
Kioni na Kega wanapigania udhibiti wa chama huku Kioni akiripotiwa kukataa kujiuzulu kutoka kwa wadhifa wa Katibu Mkuu wa chama.