BY ISAYA BURUGU  18TH MAY 2023-Chama cha Jubilee  kinasisitiza kuwa Kongamano la Wajumbe wa Kitaifa lililopangwa bado litaendelea.Katika taarifa yake, kaimu mkurugenzi mtendaji wa chama hicho Polycarp Hinga alisema NDC itaendelea kama ilivyopangwa Mei 22.

Hinga, hata hivyo, hakuzungumzia suala la ukumbi utakaoandaa.Chama hicho pia kimewaonya wananchi dhidi ya kulaghaiwa pesa na watu wasiojulikana ambao inadaiwa wamekuwa wakiomba watu walipe ili wajumuishwe kuwa wajumbe wa chama hicho.

Taarifa ya katibu mkuu Jeremiah Kioni ilisema chama hicho kina wanachama wake wanaojulikana na hakikusanyi pesa kwa ajili ya shughuli hiyo.Haya yanajiri saa chache baada ya kuchipuka kwa barua inayodaiwa kutoka Bomas of Kenya kunyima chama hicho nafasi ya kutumia ukumbi wake kwa kongamano la NDC.

Barua hiyo ilidai kuwa ukumbi wa Bomas utakuwa unafanyiwa ukarabati na hivyo hauwezi kutumiwa kwa shughuli zozote.

 

 

May 18, 2023