Chama cha Jubilee kinatarajiwa kuandaa Kongamano Maalum la Wajumbe wake mwezi Mei tarehe 22 mwaka huu.

Katika notisi iliyotiwa saini na kiongozi wa chama na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, chama hicho kilieleza ajenda kuu ya mkutano huo ni  kutunga na kuidhinisha sera za chama.

Notisi hiyo pia iliwekwa kwenye ukurasa wa Twitter wa chama hicho. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Bomas of Kenya kuanzia saa nne asubuhi.

Mapema wiki hii, chama hicho kiliamriwa kuondoka katika majengo wanayotumia sasa kama makao makuu ya chama baada ya mirengo miwili ya Kanini Kega na aliyekuwa Mbunge wa Ndaragwa Jeremiah Kioni kuzozana kuhusu uongozi wa chama.

April 29, 2023