Wakenya sasa wana uwezo wa kupata vyeti vya ndoa mtandaoni. Hii ni baada ya serikali kuondeza huduma hii kwenye mtandao wa E-Citizen, kama moja ya huduma za serikali zinazpotikana mtandaoni kwa sasa.
Katibu mkuu katika wizara ya uhamiaji na maswala ya huduma kwa wananchi Prof. Paul Bitok amesema kwamba sasa itakua rahisi kwa watu wawili waliokubali kuishi kama wanandoa kupata cheti hiki badaa ya kujaza taarifa zao kwenye mtandao huo na kufanya mahojiano ya ana kwa ana.
Akizungumza katika kaunti ya Nakuru, Bitok ameeleza kwamba huduma zaidi ya 5,000 za serikali zinaweza kupatikana kupitia rununu huku serikali ikipania kuogeza idadi hiyo ifikapo mwezi wa sita.