Shughuli za kawaida katika chuo kikuu cha Pwani zimesitishwa, na chuo hicho kufungwa kuanzia hii leo hadi tarehe 17 mwezi huu, kufuatia mkasa wa ajali ya barabara iliyosababisha mauko ya wanafunzi wa chuo hicho eneo la Naivasha.
Usimamizi wa chuo hicho umeweka peupe kwamba umetoa muda huu, ili kuwapa wanafunzi na wafanyakazi wengine chuoni humo wakati wa kuomboleza kufuatia ajali hiyo.
Naibu chansella wa chuo hicho Prof Mohammad Rajab, alieleza kwamba wanafunzi wamepewa muda huu ili kuwawezesha kupata ushauri nasaha kufuatia taarifa hizo za kusikitisha.
Basi la chuo hicho lilihusika katika ajali mbaya ya barabarani eneo la Naivasha, ajali iliyosababisha kifo cha watu 17 wakiwemo wanafunzi.