Kenya imepata inspekta jenerali mpya baada ya miezi miwili kufuatia kuapishwa na kusimikwa rasmi kwa Douglas Kanja hii leo katika ikulu ya Nairobi.

Kwenye hotuba yake wakati wa hafla hiyo ya kusimikwa kwa Kanja na ambayo imehuduriwa na viongozi mbalimbali serikalini, mkuu wa nchi rais William Ruto, ameelezea Imani yake kwa Kanja akisema kuwa uzoefu wake wa miongo minne katika masuala ya usalama, utakuwa kiungo muhimu katika kutekeleza majukumu yake kwa ueledi.

Vilevile alimweleza kuwa ana jukumu la kulinda NPS dhidi ya vitisho au ubadhirifu na kuhakikisha kwamba  sheria za nchi zinaheshimiwa bila ya kuzingatia cheo cha mtu.

Investiture of rank to the Inspector General of Police, State House, Nairobi https://t.co/kGWbjhzeR1

September 19, 2024

Leave a Comment