BY ISAYA BURUGU 27TH DEC 2022-Mkurugenzi mkuu wa mashataka ya umma Noordin Haji amewasilisha rufaa mahakamani akipinga hatua ya hakimu mkuu Douglas Ogoti kumwachilia aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko katika kesi ya ufisadi wa shilingi milioni 20 iliyokuwa ikimwandama.
Hakimu Ogoti mnamo deseimba tarehe 21 alitupilia mbali kesi dhidi ya SONKO na mtuhumiwa mwenzake Antony Ombok .Wawili hao walikuwa wanakumbwa na mshatak 13 yanayohusiana na kesi hiyo.
Hakimu Ogot alitaja ukosefu wa ushahidi kama sababu yah atua yake.DPP Haji hata hivyo anasema hakimu Ogot katika kutoa uamuzi huo alitegemea stakabadhi za zamani zilizowasilishwa tarehe 27 Januari mwaka 20202 na kupuuza zile zilizowasilishwa tarehe 7 septemba mwaka huo ambazo anasema ndizo zilizoelezea uzito kwa kesi hiyo.
Kwa mjibu wa Haji Hakimu Ogot alikosea kisheria alipotangaza kuwa mashataka hayo yalikuwa na kasoro licha yake kukubali stakabadhi mpya zilziofanyiwa marekebisho kuhusu kesi hiyo.
Sasa Haji anataka mahakama ya rufaa kutupilia mbali uamuzi huo wa hakimu Ogoti na kuagiza SONKO na wenzake kujitetea mahakamani.