Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi nchini (EACC) imetoa agizo kwa Serikali ya Kaunti ya Kilifi kusimamisha malipo ya shilingi milioni 103 kuhusiana na zabuni ya kununua mfumo wa usimamizi wa ukusanyaji mapato.

Kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwa Gavana wa Kaunti ya Kilifi, Gideon Mungaro, EACC inaituhumu kaunti hiyo kwa kuingia katika makubaliano kuhusu zabuni hiyo licha ya kuwa na onyo lililotolewa mnamo Agosti 11, mwaka huu.

EACC inaendesha uchunguzi kuhusu tuhuma za ukiukwaji wa taratibu za ununuzi wa mfumo huo, na uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mzabuni aliyefaulu hana uwezo wala uzoefu unaohitajika katika kusimamia na kukusanya mapato.

Taarifa iliyochapishwa na Tume ya EACC kuhusu Kandarasi ya mfumo wa ukusanyaji Mapato katika kaunti ya Kilifi.

October 24, 2023