Tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC imetoa wito wa ushirikiano kati ya tume hiyo na wananchi ili kukabili visa vya ufisadi humu nchini. Akizungumza katika kaunti ya Murang’a wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya kupambana na ufisadi ulimwenguni, mwenyekiti wa EACC Dkt. David Oginde amewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili wanapotekeleza majukumu yao kwa wananchi na kujiepusha na masuala ya ufisadi.
Kwa upande wake afisa mkuu mtendaji wa EACC Twalib Mbarak ameeleza kuwa ufisadi hauwezi ukatokomezwa humu nchini bila ya wananchi kushirikiana na asasi za kupambana na ufisadi.
Dr. David Oginde, Chairperson EACC: “Corruption is the single most dangerous thing that threatens our very existence as a nation. And so I agree with Kiraitu Murungi that the fight against corruption is a matter of life and death.” #UnitedAgainstCorruptionKE… pic.twitter.com/dPMUqyAR6I
— EACC (@EACCKenya) December 9, 2023
EACC Chairperson, Dr David Oginde: “Public officers should embrace integrity in their lifestyles as contemplated in our Constitution.”#UnitedAgainstCorruptionKE#IACD2023
— EACC (@EACCKenya) December 9, 2023