BY ISAYA BURUGU,15TH MARCH,2023-Tume ya maadili na kukabiliana ufisadi EACC imewaonya wahasibu wa kaunti kuhusu matumizi yasiyofaa ya mfumo wa ulipaji fedha.Kwenye notisi kutoka kwa afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Twalib Mbarak amewaonya mahasibu hao akiwagiza kuhakikisha kuwa mifumo bora itakayohakikisha kuwepo kwa uwazi katika ulipaji wa fedha umewekwa kikamilifu.
Mfumo wenye dosari unahusu malipo ya mapema wanayopewa wafanyikazi mbali mbali na maafisa wa kaunti ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao rasmi.Baadhi ya vitendo vya ukiukaji maadili vilivyogunduliwa Katika kuteleza malipo hayo ni ulipaji fedha kwa njia ya mikono bila kutumia mfumo hitajika au kuwepo mifumo miwili ya ulipaji fedha hizo kwa wakati mmoja.
EACC inasema baadhi ya maafisa huidhinisha malipo hayo kwa niaba ya wenzao ,huku maombi ya fedha hizo yakihidhinishwa bila kufuata utaratibu unaohitajika.